Home Mchanganyiko IGP SIRRO AWATAKIWA WANANCHI KUDUMISHA AMANI

IGP SIRRO AWATAKIWA WANANCHI KUDUMISHA AMANI

0

*************************************

04/09/2020 PEMBA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema hakuna kikundi cha watu wachache watakaozuia baadhi ya watu wasipige kura huku akiwataka wasijiingize kwenye uhalifu na kwamba Jeshi la Polisi litawashughulikia kwa mujibu wa sheria

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa Kisiwani Pemba ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake kisiwani humo ambapo aliwataka wadau wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kuendelea kudumisha amani na utulivu wakati kisiwani humo hasa wakati huu wa uchaguzi.

Kwa upande wake mdau wa siasa wilaya ya Chake chake, Hamisi A. Hamisi amesema hadi sasa kuna baadhi ya watu ambao wametangaza kuvuruga amani na kufanya vurugu wakati wa uchaguzi na kulitaka Jeshi la Polisi kuchunguza na kuwachukulie hatua za kisheria watu hao.

Naye mchungaji wa kanisa la Kianglikana Michael Afidhi,  ameonya baadhi ya watu kisiwani humo kuacha malumbano ya kisiasa na kudumisha amani hususani kipindi hiki cha uchaguzi.

Katika hatua nyingine IGP Sirro amewapandisha vyeo askari watatu kutoka koplo wa Polisi na kuwa Sajini wa Polisi kutokana na utendaji kazi wao mzuri wa kazi za Kipolisi.