Home Michezo KMC FC YAENDELEA KUJIFUA KUELEKEA LIGI KUU DHIDI YA MBEYA CITY

KMC FC YAENDELEA KUJIFUA KUELEKEA LIGI KUU DHIDI YA MBEYA CITY

0

…………………………………………………………

Timu ya mpira wa miguu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC inaendelea kujifua katika mazoezi yake ikiwa ni katika hatua ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania baraza inayoanza Septemba sita  mwaka huu.

Katika msimu huo wa ligi, timu ya  KMC FC itaanza mchezo wake wa kwanza siku ya Jumatatu Septemba saba mwaka huu katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo itakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Kocha wa timu hiyo, Habibu Kikwayu amesema kuwa kikosi chake kipo vizuri na kwamba wapo tayari kwa  mtanange huo katika kuhakikisha kuwa wanakuwa mabingwa kwenye msimu  wa ligi 2020/2021 .

Ameongeza kuwa katika maandalizi hayo wameweza kuboresha kikosi hicho ikiwa ni pamoja na kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita na kwamba katika msimu huu timu hiyo imekuwa na maboresho makubwa.

Amefafanua kuwa katika maandalizi hayo timu hiyo imecheza michezo ya kirafiki    nane ambayo ni timu ya DTB Bank, Kagera sugar, Namungo, JKT Tanzania, Polisi Azam pamoja na Simba.