Home Siasa MNEC HAJJI JUMAA AMPA MAKAVU TUNDU LISSU,ADAI SIASA IMEMKATAA

MNEC HAJJI JUMAA AMPA MAKAVU TUNDU LISSU,ADAI SIASA IMEMKATAA

0
…………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM Taifa, (MNEC) mkoani Pwani, Hajji Jumaa amempa makavu mgombea urais kupitia CHADEMA ,Tundu lissu kwa kudai siasa imemkataa,Watanzania wameamua kujenga nchi yao iwe kwa jasho ,kodi ama kupiga kura,kwa mgombea wa CCM ifikapo oktoba mwaka huu.
Ameeleza, wapinzani wajue uchaguzi kwa wana CCM ni sikuu ya kwenda kuinua ukuu wa Mtanzania,ni siku ya kwenda kuliinda Rasimali  za nchi yetu kwa faida ya wote kupitia sanduku la kura.
Hajji aliwaasa watanzania ,wana Pwani wafahamu kuwa Tanzania ni Taifa teule tuamke, Mungu ametuletea Mtumishi wake dkt .John Magufuli mgombea Urais kupitia CCM ,tumshike ili atupeleke kwenye nchi ya utekelezaji.
Aliwataka watanzania wasifanye makosa siku ya uchaguzi ,wachague mafiga matatu kwa kuchagua madiwani,wabunge na Rais .
“Kupigia kura  Chadema ni Kukaribisha chukizo la Mungu na Laana juu yetu,kwakuwa wao washamua kukaa kwenye upande Shetani kuruhusu Ndoa ya Jinsia moja katika Nchi yetu Tukufu, hili hatuwezi kuliachia ,nchi yetu haiwezi ikawa sehemu ya kuasi asili ya Mwanadamu kwa kisingizio Cha Demokrasia'”alisema Hajji.
Anaeleza, kazi kubwa na muelekeo wa CCM ni kwenda kuwa nchi ya viwanda vya kusadikika na kufikirika,tunataka kutengeneza magari yetu hapa,kutengeneza simu zetu ,tunataka kutengeneza saa zetu zitengenezwe ,madawa , kila kitu tufanye wenyewe na ziada viuzwe nje.