Home Siasa MGOMBEA UDIWANI KIBUTA AMPA TANO JPM

MGOMBEA UDIWANI KIBUTA AMPA TANO JPM

0
……………………………………………………..
MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
MGOMBEA Udiwani Kata ya Kibuta Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani Mohamed Kilumbi, ampa tano Rais Dkt. John Magufuli kupitia TAMISEMI kwa kuipatia kata hiyo shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.
Kiasi hicho kilitolewa na Rais kupitia TAMISEMI ambapo zimeboresha miundombinu ya shule ya sekondari ya Kata hiyo,Jokate Mwegelo  ya kidato cha tano, itayoanza kuchukua kidato cha kwanza mwaka huu.
Shule hiyo imepewa jina hilo kutokana na juhudi za Mkuu huyo za harambee iliyoandaa, ikifanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo fedha hizo zimejenga shule hiyo hatua inayolenga kutokomeza ziro walayani humo.
“Sanjali na shukrani kwa Rais John Magufuli, pia tunampongeza Mbunge wetu Suleiman Jafo Waziri wa TAMISEMI, kwa kazi kubwa anayoifanya ambapo kupitia ofisi hiyo ametupatia kiasi hicho cha fedha zilizopelekwa kwenye shule yetu ya Kata,” alisema Kilumbi.
Pia amezungumzia kauli ya Rais Magufuli ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami inayoelekea mbuga ya Serou (Nyerere National Park) ambayo itaendelea kufungua njia za kiuchumi, sanjali na maji ya mto wami yanayotaraji kupita katika vijiji mbalimbali.
“Mbali ya shule hiyo ya Joketi, Rais Magufuli kupitia TAMISEMI wizara inayosimamiwa na Mbunge wetu Jafo, imetupatia shilingi milioni 300 tumeboresha majengo katika shule yetu, tumchague kwa kura nyingi Rais wetu,  Mbunge Jafo na mimi,” alisema Kilumbi.
Akizungumzia elimu ya msingi alisema alipochaguliwa Kata ilikuwa ya 15 kati ya shule 17, waliweka kambi na akichagia kilo 500 za mahindi, aliwezesha uchapishaji, huku walimu wakifundisha kwa umahiri mkubwa hatimae mwaka 2019/2020 imeshika ya 5 kati ya 17.
Kwa upande wake Msafiri Mpendu mtia nia udiwani Kata ya Marumbo alisema kuwa Kilumbi ni chaguo sahihi, na kwamba wana mpango wa kuifungua barabara ya Muhaga kuelekea Marumbo kwa gharama zao wenyewe.
“Niwaombe wana-Kibuta tumchague Kumbi, kwani ni chaguo sahihi, tunaona juhudi zake ameanza ujenzi wa stendi na soko kwa gharama zake nani anaweza hilo?,” alisema Mpendu.
Awali Mohamed Masenga na Mwalimu Said Kikwayu walisema kuwa wagombea wanaotokea ndani ya Chama Cha Mapinduzi wana kila aina ya sifa hivyo wasipoteze fursa hiyo.