Home Siasa CHAMA CHA ACT WAZALENDO KIMEZINDUA ILANI YA CHAMA HICHO 2020

CHAMA CHA ACT WAZALENDO KIMEZINDUA ILANI YA CHAMA HICHO 2020

0

**************************************

Chama Cha ACT Wazalendo leo kimezindua ilani ya chama hicho 2020 ambapo imebeba ajenda 11 zitakazonadiwa katika kameni za uchaguzi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Mshauri wa chama hicho ambae pia ni mgombea uraic wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benard Membe amesema atainadi ilani hiyo nchi nzima.

Amesema kuwa, tangu aanze kushiriki katika uchaguzi hajawahi kukutana na ilani ambayo imetekelzwa kwa kukidhi mahitaji ya wananchi kama ilani ya ACT Wazalendo ya mwaka 2020.

“Hata huko niliko toka ilani yao ya chama ilikua imetekelezwa kwa asilimia 31endapo wananchi wataichagua ACT Wazalendo hizo zilizobakia asilimia 69 zitatekelezwa ACT Wazalendo”amesema Membe.

Ameongeza kuwa, wamedhamiria kutekeleza ajenda zote zilizopo katika ilani hiyo, pia watajali usawa wa kijinsia endapo wanawake watashindana kwenye uchaguzi wataingia bungeni bila kupingwa.