**********************************
EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa kombe la Ngao ya Hisani dhidi ya Namungo Fc kwa kuwatundika mabao 2:0 katika uwanja wa Abeid Amani Karume Jijini Arusha.
Bao la kwanza lilifungwa na Mshambuliaji wao mahiri John Rafael Bocco kwa mkwaju wa penati baada ya kiungo mshumbulia wao mpya Bernad Morrison kuchezewa rafu ndani ya kumi na nane.
Bao la pili lilifungwa na Bernard Morrison ambaye alionyesha kiwango kikubwa kwa mchezo huo kwani alifanikiwa kusababisha bao la kwanza na kupachika bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2:0.