Home Michezo ROUND 10, ZA MTOSHA TWAHA KIDUKU KUMTIFUA DULLA MBABE ULINGONI

ROUND 10, ZA MTOSHA TWAHA KIDUKU KUMTIFUA DULLA MBABE ULINGONI

0

********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Twaha Kiduku fahari ya Morogoro ameshinda pambano lake dhidi ya Dullah Mbabe lililopigwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baada ya raundi 10 kupigwa, majaji wote watatu walimpa ushindi Twaha Kiduku wa 93-97, 91-99 na 93-97.

Mashabiki wengi walifurika kushuhudia pambano hilo la aina yake baada ya kutambiana kila mmoja kuonesha mbabe zaidi ya mwenzake.