Home Mchanganyiko TWARIQA TANZANIA  KUONGOZA WAISLAMU  SHINYANGA KUOMBEA AMANI  AUGUST 29

TWARIQA TANZANIA  KUONGOZA WAISLAMU  SHINYANGA KUOMBEA AMANI  AUGUST 29

0
Sheikh Aboubakari akizungumza na Viongozi wa Twariqa Taifa waliofika kumtembelea katika chuo chake Cha Kiislamu mtaa wa majengo mkoani shinyanga.
Viongozi wa Twariqa Taifa na Viongozi wa Twariqa mkoa wa shinyanga katika picha ya Pamoja na Baadhi ya wanafunzi wa chuo Cha Kiislamu.
Wanafunzi wanaosoma dini ya Kiislamu katika chuo Cha Sheikh Aboubakari kilichopo mtaa wa majengo mkoani shinyanga Wakisikiliza Mawaidha ya Viongozi wakuu wa Twariqa Tanzania ambao hawapo pichani.
Msemaji wa Taasisi ya Twariqa Tanzania Shekhe Haruna Hussein Kushoto akiwa  na Darueshi Musa kutoka Uganda wakifurahia Jambo mkoani Shinyanga.
…………………………………………………………………
Na.Mwandishi Wetu -Shinyanga.
Wailsamu wametakiwa kuungana na kushirikiana katika kuwekeza  ndani ya jamii katika sekta Mbali Mbali,bila kujali Itikadi za kidini  ili kuhakikisha kuwa dini ya Kiislamu inasonga mbele.
Hayo yameelezwa na Msemaji wa Taasisi Kongwe ya dini ya Kiislamu nchini ya Twariqa Shekhe Haruna Hussein,wakati akizungumza na wanachuo wa Chuo Cha Kiislamu kinachofahamika  Cha  Shekhe Aboubakari kilichopo Majengo Mapya mkoani Shinyanga.
Shekhe Haruna alisema kuwa katika kuwa ni vyema Waislamu wanatumia Neema Mbali Mbali vizuri ili kuhakikisha kuwa jamii inanufaika na dini lakini pia huduma Mbali mbali za kijamii kama shule,hospitali na nyinginezo.
“Tusiangalie Itikadi tulizonazo na msikae kinyonge Sana,tuipeleke dini mbele na ule mfumo wa Waislamu kusimama ufike mwisho Sasa,na viongozi wa Dini ya Kiislamu mguswe na matatizo ya Watanzania”alisema Shekhe Haruna.
Aidha aliwataka Viongozi wa Kiislamu kwenda Mbali Zaidi na kuacha kasumba ya kugombania Sadaka misikitini,badala yake wajenge zawia za kutosha ili kuhakikisha kuwa maadili hayapotei ndani ya jamii.
Nae Katibu Mkuu wa Twariqa Tanzania Yahya Athman Mkindi alisema kuwa ujio wa viongozi wakuu wa Twariqa Tanzania katika mkoa wa shinyanga ni maandalizi ya Kongamano kubwa la Amani linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya  Masjid Firdaus Ngokolo B,August 29.
Shekhe Mkindi alisema kuwa Kongamano hilo litaambatana na Harambee kwa ajili ya kiwanja Cha Zawiya na Markaz.
Katibu huyo alisema kuwa lengo la Kongamano hilo Ni kuombea Amani Taifa katika kuelekea Uchaguzi mkuu wa October 28,lakini pia kuwaasaa wagombea wa vyama vyote ambavyo vinashiriki uchaguzi kufanya kampeni za kistaarabu.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo inasema kuwa “Uchaguzi Mkuu bila Vurugu Inawezekana”.