Home Mchanganyiko Padri Sanka wa Shirika la Wapalotini Amezikwa Leo Galapo Babati

Padri Sanka wa Shirika la Wapalotini Amezikwa Leo Galapo Babati

0

……………………………………………………………………….

Na John Walter-Manyara

Mwili wa aliyekuwa Padri wa Shirika la Wapalotini  Padri Victor Sanka umepumzishwa Leo agosti 28,2020 katika makaburi ya Wapalotini yaliyopo katika Parokia ya  Galapo wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Padri Victor Sanka amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Sanka ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha  Bashnet wilayani Babati Mkoa wa Manyara,  ni kati ya walelewa wa kwanza waliojiunga na shirika la Wapalotini.

Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu Antony Lagwen amewaambia mamia ya waombolezaji waliofika katika ibada ya kumsindikiza kwenye nyumba ya milele, wamuenzi Padri Sanka kwa kutenda yale  yaliyo mema.

Padri Sanka alifariki dunia agosti 22,2020 katika hospitali ya Buma iliyopo Bashnet alipokuwa akipatiwa matibabu.

Raha ya ya milele umpe ee Bwana, Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa Amani,Amen.