Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemkabidhi Meja Jenerali wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Charles Mbuge fedha za kitanzania Shilingi Milion 30 kutoka kwa wadau kwaajili ya ujenzi wa Msikiti Chamwino.
Fedha hizo zilichangishwa siku ya jana katika Tamasha la Jumuiya ya maridhiano liliofanyika katika uwanja wa jamhuri Jijini hapa.
Akikabidhi fedha hizo kwa Meja Jenerali Mbuge katika ukumbi wa mikutano uliopo Mkoani hapa,Dkt Mahenge amesema wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kutoa michango yao na wengine kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa msikiti kuko Chamwino.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum amesema Rais John Magufuli amefanya Jambo jema kwa wananchi wake wa dini ya Kislamu.
” Kwaniaba ya Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakari Bin Zuberi nimeongea na amekiri kwamba amefurahishwa na Rais Magufuli kuwatafutia wananchi wake nyumba ya Ibada na ameahidi kuja kutembelea,”amesema Alhadi Salum.
Na kuongeza kusema ” Tunamuombea Rais wetu awe na maisha marefu na wale wote wanaomuunga mkono na kumsaidia Rais wetu,” Amesema.
Akiongea baada ya kukabidhiwa fedha hizo Meja Jenerali wa Jeshi la kujenga Taifa Charles Mbuge amewapongeza viongozi wa dini kuwa na upendo na mashikamano ya pamoja.
Amesema hiyo yote inatokana na Amani na utulivu tuliokuwa nao ndani ya Nchi yetu na ndio mana tunasali tunatembea tukiwa na Amani.
” Naomba tu niseme tunaelekea kipindi Cha uchaguzi tudumishe Amani na mshikamano na tuwe pamoja na tumalize uchaguzi salama bila ya machafuko,”amesema Mbuge.
Hata hivyo aliwataja wadau waliochangia Ujenzi huo wa Msikiti nipamoja na Azim Dewji Mwenyekiti Kitosa Shia Ithna Shilingi Milion 10 keshi.
Abdul Zacharia,kutoka Abdul Zacharia Al Naeem Enterprise LTD ametoa Milion 20 keshi
Na Shekhe Arif Nahd Mwenyekiti Islamic Foundation ameahidi Shilingi Milion 10,005,000 na Jeshi la kujenga Taifa kuahidi Shilingi Milion 5.