Home Mchanganyiko Guavay Co Ltd Yatoa mafunzo kwa Wasimamizi wa Mashamba Ya Parachichi Njombe

Guavay Co Ltd Yatoa mafunzo kwa Wasimamizi wa Mashamba Ya Parachichi Njombe

0

***************************

Na Joctan Myefu 

NJOMBE   ,
Takriban wasimamizi(farm manager) 70 kutoka makampuni tofauti ya mashamba ya parachichi yenye ukubwa za zaidi ya hekta 900 mkoani Njombe wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya kilimo hai na kampuni ya GUAVAY COMPANY LIMITED ili kuongeza thamani na ubora utakaokuwa na ushindani katika soko la ndani na nje ya Tanzania.

Licha ya takwimu kuonyesha kuwa Tanzania inazalisha zaidi ya Tani elfu 8 hadi 9 kwa mwaka na Kenya kuzalisha tani elfu 90 kwa mwaka lakini bado malighafi inayozalishwa nchini bado imekuwa na changamoto sokoni kwa kuwa wakulima wengine wamekuwa wakitumia kemikali katika kilimo hatua ambayo inatajwa kuwa na athari kwa walaji na kulazimika kupendelea mazao ya oganiki.

Huyu hapa mkurugenzi wa kampuni ya GUAVAY COMPANY LIMITED Ahadi Katela anaeleza sababu ya kujikita katika kutoa elimu ya kilimo hai kwa wakulima ili kutengeneza soko la uhakika ndani na nje ya Tanzania

Christina Myonga msimamizi wa shamba la shule ya sekondari Mtwango na Yohanes Nyawike  ni baadhi ya wanufaika wa mafunzo ya kilimo hai ambao wanasema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata mazao duni kutokana na kutozingatia taratibu za kilimo hicho na kwamba elimu hiyo inawafanya kwenda kufanya mapinduzi huku pia wakiomba wataalam wa serikali na taasisi za kilimo kuendelea kuwatembelea na kuwaelimisha.

Nae muwezeshaji wa mafunzo hayo Musa Joshua amesema mbali na kutoa elimu kwa wasimamizi lakini amewashauri wawekezaji wakubwa na wadogo kuhakikisha wanaweka mazingira bora na rafiki kwa mnunuzi na mfanyakazi ili kuongeza hamasa kwa wengine .