Na John Walter-Manyara
Flatei Gregory Massay aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbulu vijijini akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Ndg. Hudson Kamoga leo Agosti 22, 2020.
Flatei ambaye alipata fursa tena ya kugombea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na wajumbe, amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Mbulu vijijini Mkoani Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha mwaka 2020-2025.
Ikumbukwe kwamba, Uchaguzi Mkuu wa kuchagua madiwani,Wabunge na Rais utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
Kampeni za uchaguzi mkuu zitaanza rasmi tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.