Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania itaipamba fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Bayern Munich na Paris Saint- Germain kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa mashabiki wa soka watakaojibu maswali mbalimbali.
Timu hizo zitakutana kwa mara ya kwanza Jumapili (Agosti 23) kwenye uwanja wa Estadio da Luz wa Ureno i wenye uwazo wa kuingiza watazamaji 64,642 na M-Bet imeandaa kumbi mbili, Samaki Samaki Mlimani City na Masaki ambapo watafunga ‘screen kubwa’ kwa ajili kwa ajiliya kuonyesha mpira huo.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema jana kuwa mbali ya kuendesha chemsha bongo inayolenga mechi hiyo na historia ya mashindano ya Champions League, pia burudani mbalimbali zitakuwepo kwa ajili ya kuburudisha mashabiki.
Mushi amesema kuwa wamefanya hivyo ili kuwakutanisha mashabiki wa soka na mbali ya kuangalia mechi, pia watajumuika pamoja na kubadilishana mawazo.
“Hii ni moja ya mikakati ya M-Bet Tanzania kuwakutanisha mashabiki pamoja na kujumuika kuangalia fainali hiyo ambapo zawadi kama za mipira, jezi, fulana na nyinginezo nyingi zitatolewa kwa wataojibu maswali ya fainali ya mechi hiyo na historia ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya,” alisema Mushi.
Alisema pia kutakuwa na maswali yahusiyo kampuni yao ambayo imefanikiwa kutoa washindi wengi na kuwazawadia zawadi mbalimbali ambazo zimeweza kubadili maisha yao.