Home Mchanganyiko MIZINGA YA NYUKI KUDHIBITI TEMBO WASIINGIE MASHAMBA YA BAGAMOYO SUGAR

MIZINGA YA NYUKI KUDHIBITI TEMBO WASIINGIE MASHAMBA YA BAGAMOYO SUGAR

0

***********************************

NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
MIZINGA ya nyuki inatarajia kuwekwa katika mpaka wa mashamba ya Miwa ya Kampuni ya Bagamoyo Sugar, hususani upande unaopakana na Hifadhi ya Mbuga ya Saadani, ikiwa ni mikakati ya kudhibiti Tembo wasiingie katika mashamba hayo.
Shamba hilo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa Group chini ya Mkurugenzi Said Bakhresa, lina ukubwa wa hekta elfu kumi (10,000)malengo yakiwa ni uzalishaji wa sukari,ambapo kwa sasa ujenzi wa majengo mbalimbali unaendelea.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Makampuni hayo Hussein Sufiani, wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa amekwenda kutembelea eneo la mradi huo.
Kauli ya Sufiani imetanguliwa na swali lililoulizwa na Mhandisi Ndikilo, aliyeanza kwa kusema akiwa Mkuu wa wilaya katika moja ya wilaya mkoani Morogoro kulikuwa na changamoto kubwa ya tembo kuingia kwenye mashamba ya miwa, huku akitaka kujua mikakati ya Kampuni.
Akielezea ujenzi wa mradi huo unaojengwa kwa awamu tofauti, anasema tayari wa-Tanzania 600 wananufaika na mradi, ambapo alieleza kuwa uzalishaji utakapoanza kwa msimu wanatarajia kuzalisha tani 35,000.
“Katika kujihami na matukio ya Tembo kuingia ndani ya mashamba yetu kula miwa tumejipanga kikamilifu, tunataraji kuandaa mizinga ya nyuki itayowekwa katika miti kando ya mashamba yetu na Hifadhi ya Taifa ya Saadani, nadhani hiyo itakuwa hatua nzuri ya kuwadhibiti wanyama hao hatari” alisema Sufiani.
Sufiani alifafanua, wanatarajia kusaidia ongezeko la uchumi kwa wana-Bagamoyo, Mkoa na nchi kwa ujumla.
Nae Ndikilo alisema,Rais Magufuli ameamua kuupatia uongozi wa Kampuni hiyo eneo hilo kwa lengo la kuendelezwa kwa kilimo cha miwa, juhudi ambazo zimeshaanza kuleta matunda kwa wana-Bagamoyo, Mkoa na nchi kwa ujumla kutokana na kuwepo kwa wa-Tanzania 600 waliotangulia kunufaika kupitia mradi huo.
Alielezea,matunda ya Rais Magufuli kuipatia ardhi Kampuni ya Bakhresa Group yanaanza kuonekanna, kwani mbali ya kuwepo kwa ajira ya kutosha pia uzalishaji huu utaotengeneza upatikanaaji wa sukari hapa nchini.