Home Mchanganyiko DKT. GWAJIMA AWATAKA WAKURUGENZI WOTE WA HALMASHAURI KUZISIMAMIA KWA KARIBU TIMU ZA...

DKT. GWAJIMA AWATAKA WAKURUGENZI WOTE WA HALMASHAURI KUZISIMAMIA KWA KARIBU TIMU ZA AFYA.

0

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Timu ya Afya Mkoa wa Simiyu (haipo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo hivi karibuni.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange wakati wa kikao na Timu ya Afya ya Mkoa wa Simiyu hivi karibuni.Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akizungumza wakati alipopokea ugeni wa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima hivi karibuni. 

Timu ya Afya ya Mkoa wa Simiyu(RHMT) wakiwa katika kikao kazi na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa ziarani Mkoani Simiyu hivi karibuni

……………………………………………

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima  amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko  kwa kujitoa katika kusukuma mabadiliko sekta ya afya kwa vitendo licha ya wataalamu wa afya waliotakiwa kusimamia kuwa wazembe kwenye utekelezaji.

Dkt. Gwajima amebainisha hayo leo Jijini Dodoma baada ya kuona Mkurugenzi huyo ameaanza kutekeleza kwa kasi kubwa maagizo aliyopewa wakati wa ziara yake wilayani humo.

Aidha Dkt. Gwajima ameeleza kuwa Mkurugenzi huyo hakusita  kufanya mabadiliko pale alipoona kasi ya utendaji wa watumishi wake  ni ndogo katika kuleta matokeo ya utendaji wao licha ya yeye mwenyewe kujitahidi sana kuwapa ushirikiano hapo awali ila hawabadiliki.

Dkt. Gwajima amesema kuwa kiongozi mzuri ni yule mwenye udhubutu wa kufanya maamuzi pale anapoona hakuna matokeo mazuri kutoka kwa watendaji hivyo Mkurungenzi huyo anastahili pongezi kwa kuwa hakusita kufanya mabadiliko ya awali kwa kushirikiana na Uongozi Mkoa. 

“Hata hivyo kutokana na utendaji wake mzuri nimefuatilia kwa ukaribu utendaji wa watumishi wake  na kubaini mazoea yamekithiri,  hatimaye kwa kushirikiana na mkoa wakaomba msaada Ofisi ya Rais TAMISEMI ambao mimi na timu yangu ya TAMISEMI tulifika  na kushuhudia

yanayojiri na baadae kuchukua hatua zaidi kwa watumishi wasiotimiza weledi wao kwa ufasaha”, ameeleza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima  ametoa wito kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuendelea kutoa ushirikiano katika kuzisimamia na kuzilea Timu za Afya za Halmashauri. Hata hivyo.

“Wakurugenzi mnatakiwa kuwa wepesi wa kung’amua iwapo timu hizo hazikidhi viwango vya uwajibikaji basi wasisite kufanya mabadiliko ya haraka sana ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano”,amewasisitiza Dkt. Gwajima.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amesema lengo ya  kasi ni utekelezaji uendane na kile ambacho wananchi wanakitaka kama ambavyo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli