Home Michezo MASHINDANO YA KUOGELEA YA HPT KUFANYIKA AGOSTI 29 MWAKA HUU

MASHINDANO YA KUOGELEA YA HPT KUFANYIKA AGOSTI 29 MWAKA HUU

0

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Mashindano  ya wazi ya kuogeleaya HPT yatafanyika Agosti 29 katika bwawa la kuogelea la shule ya sekondari ya Shaaban Robert, Upanga au (Champion Rise) jijini.

Katibu Mkuu wa Chama Cha kuogelea Tanzania  (TSA) Inviolata Itatiro alisema kuwa mashindano hayo yameandaliwa na makocha wanaofundisha waogeleaji yajulikanayo kwa jina la High Performance Training na chama chao kuwapa kibali.

Inviolata alisema kuwa TSA inatambua mchango wa wadau katika kuendeleza mchezo huo hapa nchini na wanaamini mashindano hayo yatatoa picha halisi ya maendeleo ya waogeleaji baada ya kumpumzika kwa takribani miezi miwili na nusu kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Alisema kuwa wanatarajia waogeleaji wengi kujitokeza katika mashindano hayo ambayo yatakuwa ya siku moja na kila muogeleaji anatakiwa kushindana kwenye vipengele vinne tu.

 “TSA inatambua mchango wa wadau katika kuhakikisha mchezo wa kuogelea unapata maendeleo. Hivyo mashindano ya wazi na mchnganyiko ya HPT ni ya kwanza tangu  serikali kuruhusu michezo miezi miwili iliyopita, ” alisema Inviolata.

Staili mbalimbali za kuogelea zitashindaniwa katika mashindano. Staili hizo za kuogelea ni Freestyle, Breaststroke, Butterfly, Backstroke na Individual Medley.

Alisema kuwa hata waogeleaji binafsi wameruhusiwa kushindana katika mashindano hayo yaliyopangwa kuanza saa 1.00 asubuhi mpaka saa 7 mchana.

“Tutakuwa na waogeleaji ambao watakuja na klabu zao na wengine ambao hawana wataogelea binafsi. Tumefanya hivyo  kwa lengo la kuwapa fursa waogeleaji ambao wamekuwa wakiogelea kwenye mabwawa binafsi,” alisema.

Kwa mujibu wa Inviolata, mwisho wa timu na waogeleaji binafsi kuthibitisha ni Agosti 25.

Kwa upande kocha wa HPT, Michael Livingstone alisema kuwa wamefurahi kupata ushirikiano na kutoka TSA ili kufanikisha mashindano hayo.

Livingstone amewaomba waogeleaji ambao wapo katika mafunzo yao wataogelea kama klabu moja ili kujua maendeleo yao kutokana na mfunzo waliyofanya.

“Tunefarijika sana kupata ushirikiano na TSA na kutupa kibali cha kuendesha mashindano haya, tunawaomba waogeleaji kujitokeza kwa wingi ili kupima uwezo wao,” alisema Livingstone.