Home Mchanganyiko KUSAYA AAGIZA VYUO VYOTE VYA KILIMO NCHINI  KUTENGENEZA  MAZINGIRA YA KIBIASHARA

KUSAYA AAGIZA VYUO VYOTE VYA KILIMO NCHINI  KUTENGENEZA  MAZINGIRA YA KIBIASHARA

0
MAKAMU WA RAIS AHIMIZA MATUMIZI YA STAKABADHI ZA GHALA - MSUMBA ...
Na Silivia Mchuruza, Bukoba
KATIBU mkuu Wizara ya kilimo Gelard  Kusaya ameahidi kutatua changamoto mbalimbali zilizoko ndani ya uwezo wa Serikali zinazowakabili  chuo Cha kilimo Maruku- MATI kilichoko Bukoba Vijijini mkoani Kagera hususani,maslahi ya watumishi na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia wanachuo  na kukujenga majengo mapya ya kisasa na ya mfano ili kuweka mazingira bora yatakayowavutia na kusoma kwa amani na furaha.
Aidha ameagiza vyuo vyote vya kilimo nchini kutengeneza mazingira ya kibiashara ili vyuo hivyo viweze kujitegemea kwa kujiendesha kuliko kusubiri ruzuku kama ilivyo sasa wakati wanazo raslimali ikiwemo maeneo yaliyoachwa wazi bila kuedelezwa ambayo yamekuwa mapori wakati yangetumika kuanzisha shughuli za uzalishaji na kuingiza kipato.
Akiwa ziarani Bukoba ametembelea na kukagua miundombinu na mashamba darasa chuoni hapo na kujionea maeneo ambayo yako wazi ambayo hayatumiki na kisha alipata taarifa juu ya Maendeleo ya chuo na mipango ya baadaye kutoka kwa mkuu wa chuo hicho Mathew Luhembe.
 Pia ameongea na wanachuo na  watumishi wa kada mbalimbali chuoni hapo na kusikiliza changamoto zinazowakabili ambapo aliwapa moyo kuwa zitatafutiwa majibu ya haraka  kwani Serikali ya Rais John Magufuli ipo kwa ajili ya kutoa fedha kumaliza kero za aina hiyo.
Alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha wanajenga mazingira mazuri na rafiki kwa wanachuo na watumishi wote hapa nch
Naye Sophia Christian ni mfanyakazi wa muda katika chuo hicho amemuomba  katibu mkuu kuwatizama kwa jicho la huruma wafanyakazi wa muda wasio na ajira ya kudumu kwa  kuogezewa kiasi cha malipo yao ya mwezi kwani,wanafanya kazi kubwa ukilinganisha na kiasi cha sasa wanacholipwa shilingi laki 135,000 na kulipwa kwa wakati ili kupinguza changamoto zinazowakabili za kifamilia.
Jackobo Marco ni Rais wa Serikali ya wanachuo hao alitoa shukrani kwa Katibu mkuu kwa kuwapatia gari ambapo limekuwa mkombozi kwao kwani wakati mwingine inatokea mgonjwa wa dharula hasa usiku lakini walikuwa inakuwa ngumu kupata usafiri na sasa hiyo imepungua ambapo,wameomba Serikali kuwaletea hata nesi katika mazingira yao ya chuo ili wawezekupata huduma ya kwanza wakati taratibu nyingine za kupata huduma za Afya kunakohusika.
Baada ya Katibu mkuu Kusaya kusikia hayo amewaeleza kuwa kuanzia wiki ijayo ataleta Kompyuta za kutosha,pikipiki nne ,kuwaletea nesi kwa ajili ya huduma ya kwanza kuongeza posho ya mwezi kwa wafanyakazi wa muda toka laki 135 hadi laki 200,000,kujenga bwalo la kulia chakula,kuleta ng’ombe wa kulikia na power teler na trekta itakayotumika kwa ajili ya kilimo na kujifunzia pamoja na kutatua changamoto ya mafao ya watumishi na kupandishwa vyeo .
Alisema sasa Serikali inaompango wa kujenga majengo mapya ya kisasa na mfano ya chuo hicho hivyo akaahidi wiki ijayo kutuma timu ya wataalam waje wapite maeneo ya chuo na kutoa ushauri waatumizi bora ya ardhi ni eneo gani lijengwe majengo mapya ila ninachoomba mkuu wa chuo kuwasiliana na watu wa mipango miji tupate ramani haraka tuanze taratibu kazi hiyo.
“Baada ya hayo sasa naagiza vyuo vyetu vya kilimo vipatapatavyo 14 hapa nchini na vituo vidogo vinne kuandaa utarati b u wa kujiendesha kibiashara kwa kutumia raslimali walizonazo,tunayo maeneo makubwa lakini yamebaki kuwa mapori tujenga vitega uchumi,tuanzishe mashamba darasa tukivuna mazao tukauza tunaongeza pato”aliagiza .
Wakati huo huo ametembelea Taasisi ya utafiti wa zao la kahawa (TaCRI) -Maruku ambapo ameagiza kuendelea kuzalisha Miche kinzanima na magonjwa mingi zaidi ya kahawa na kuwagawia wananchi ili waendelee kulidhika na kuongeza tija kati kuzalisha zao hilo,pia ametembelea Taasisi ya utafiti wa kilimo -TARI Maruku ambapo amewataka kuendelea kufanya tafiti zake katika mazao mbalimbali hari itakayopelekea wananchi kulima kwa ubora na tija.