Home Mchanganyiko ZIARA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WILAYA YA ARUSHA SIKU...

ZIARA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WILAYA YA ARUSHA SIKU YA KWANZA

0

******************************

Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh Kenani Kihongosi leo ameanza ziara ya kikazi kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Tarafa ya Elerai, katika Kata ya Murrieti ambapo amepokea kero mbali kutoka kwa wananchi na Kuzielekeza mamlaka husika kuzichukulia hatua na kero nyingine ameweza kuzitatua papo kwa papo, Mh kenani Amesema “Jukumu letu viongozi sio kukaa ofisini Bali ni kufika kwa wananchi wetu na Kuwatatulia kero zao, Mhehsimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli halali sasa nitashangaa kuona watumishi mnalala badala ya kwenda Kuwasikiliza wananchi,hivyo mimi ni Mtumishi wenu wana Arusha na nitawatumikia kuhakikisha tunamaliza kero zenu” Katika ziara Hiyo mkuu wa wilaya Aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji pamoja na Wataalamu wa halmashauri ya Jiji la Arusha. Ziara ya Mkuu wa Wilaya itaendele kesho Tar 11.08.2020 katika Ofisi za kata ya Murrieti.