Home Mchanganyiko WANAFUNZI CHUO KIKUU TUMAINI DAR ES SALAM WAPIGWA MSASA NA MISA TANZANIA...

WANAFUNZI CHUO KIKUU TUMAINI DAR ES SALAM WAPIGWA MSASA NA MISA TANZANIA KUHUSU SHERIA ZA MTANDAONI

0

Mkufunzi akiendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea fani ya uandishi wa habari katika chuo kikuu cha Tumaini Jijini Dar es salaamNA FREDY MGUNDA, DAR ES SALAM.

WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salam idara ya uandishi wa habari wapigwa msasa na Taasisi ya Vyombo vya
Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kuwaongezea upeo wa elimu
ya uandishi wa habari katika nyanja mbalimbali za taaluma hiyo.

 


Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo mkufunzi wa sheria za vyombo vya habari
Adv. Deogratius Bwire alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea
uwezo wa kuitambua vizuri taalum hiyo ili wakihitimu masomo wanatakiwa
kwenda kutumia taalum hiyo kwa kufuata misingi na kanuni walizopewa wakiwa
chuoni.


Alisema kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuzijua sheria zilizopo katika
sekta ya habari
na kuendana na sayansi na teknolojia ambayo imekuwa na mabadiliko ya
mara kwa mara.“Tunatoa elimu hii kwa lengo la kuongeza uelewa na kwa wanafunzi hao wa
vyuo vikuu ili wakihitimu masomo yao waende wakafanye kazi ya uandishi wa
habari kwa weredi 
unaotakiwa kwa kuifanya tansinia hii kuwa imara na yenye wasomi wanaofuata
maadili,kanuni,sheria 
na katiba ya nchi” alisema.

 

Alisema kuwa waandishi wengi wa habari bado hawazijui sheria mpya za
mitandao ya kijamii hivyo waandishi wanatakiwa kusoma kila mara ili kupukana na
sheria ambazo zinakuwa zinatungwa kwenye tansia ya habari.

 

Bwire aliongeza kuwa wananchi wengi hawajui hizi sheria za mitandoa ya
kijamii na ndio maana saizi kumetokea kwa wananchi wengi wanapelekwa mahakamani
kwa kutukujua sheria hizi za mitandao ya kijamii.

 

“Kumekuwa na wimbi kubwa hizi karibuni kwa waandishi wa habari
wamekumbana na kuanzisha maudhui ya kihabari mtandaoni kinyume cha sheria za
mitandaoni ambazo zimetungwa hivi karibuni bungeni na kupitishwa na Rais wa
Jamhuli ya Muungano wa Tanzania na sasa zinatumika hivyo umakini unatakiwa sana”
alisema

 

 

Aliongeza kuwa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa

Afrika (MISA) tawi la Tanzania imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara
kwa waandishi wa habari mbalimbali kwa lengo la kumsaidia mwandishi wa habari azitambue
haki zake na kujitambua mwenyewe kwenye kazi yake.

 

Kwa upande wake wa mhariri wa Clouds Media Joyce Shebe aliwataka
wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari kuwa makini na uandishi wa habari kwa
kuhakikisha kuwa wanaandika habari zenye mizani sawa ili kuihabarisha jamii
habari ambayo imekamilika.

 

Shebe alisema kwenye sheria za mitandao inatakiwa kuepuka sana
kuonyesha sura za watoto au mtu aliyebakwa au kufanyiwa ukatili kutoonyesha
nyuso za wausika ili kulinda haki ya maisha yake.

 

“Waandishi mkiwa kazini mnatakiwa kufanya za uandishi wa habari kwa
kuzingatia maandili ya uandishi ili kuondoa migongano baina ya serikali na
jamiii kulingana na aina ya habari ambayo unakuwa umeifanyia kazi” alisema
Shebe

 

Nao baadhi ya wanafunzi chuo cha Tumaini Dar es Salam idara ya uandishi wa habari wamejifunza kwa namna gani wanaweza
kupambana na changamoto za tansinia ya habari kutokana naelimu ambayo wamepata
kwenye mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa siku tatu katika chuo hicho.

 


Walisema wanaendelea kujifunza misingi ya wanahabari ili kufanya kazi
kwa weredi mkubwa wenye kuzingatia misingi na sheria za taalum hiyo ambayo
imekuwa na changamoto nyingi.