Home Mchanganyiko TMDA YATUMIA GARI MAALUM LILILOCHORWA VIBONZO KUTOA ELIMU VIWANJA VYA NANENANE NYAKABINDI-SIMIYU

TMDA YATUMIA GARI MAALUM LILILOCHORWA VIBONZO KUTOA ELIMU VIWANJA VYA NANENANE NYAKABINDI-SIMIYU

0

********************************

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imetumia gari maalum lililochorwa vibonzo kutolea elimu kwa Wananchi mbalimbali waliotembelea kwenye mabanda hayo katika viwanja vya Nyakabindi, Simiyu.

Umati mkubwa wa watu umekuwa ukivutika kwa wingi katika banda la TMDA ambalo limekaa sambamba na gari hilo.

Afisa Habari na Elimu kwa Umma, James Ndege alieleza kuwa, TMDA mara kwa mara inahakikisha inabuni mbinu mbalimbali za kuhamasisha jamii juu ya wajibu wao katika kulinda afya zao.

Aidha, alisema katika kuwafikia wadau waliopo maeneo mbalimbali, Mamlaka imetoa ujumbe wa kukumbusha jamii juu ya wajibu wao kwa njia ya vibonzo ili kufikia jamii pana zaidi na kwa haraka.

Uhamasishaji huo wa vibonzo kupitia gari hilo maalum unahamasisha utoaji taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa ambayo imeonekana ni njia rahisi zaidi.

TMDA imekuwa ikitoa elimu kwa Wananchi juu ya ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaatiba na vitendanishi katika maonesho hayo ya Nanenane ambapo msimu huu ni mwaka wa tatu mfululizo yakifanyika Kitaifa kwenye viwanja hivyo vya Nyakabindi, Simiyu.