Home Siasa MGOMBEA URAIS ACHUKUA FOMU ‘PEKU BILA VIATU’,UPDP ,ADC NAO WAJITOSA KUWANIA KITI...

MGOMBEA URAIS ACHUKUA FOMU ‘PEKU BILA VIATU’,UPDP ,ADC NAO WAJITOSA KUWANIA KITI HICHO

0

Mgombea Uraiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Sauti ya Umma SAU Bw.Mutamwega Mgaiwa akiwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma akiwa peku bila viatu alipoenda kuchukua Fomu ya kuwania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.

Mgombea wa Urais ,Mutamwega Mgaiwa akikabidhiwa Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Sauti ya Umma SAU katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Mutamwega Mgaiwa wakionyesha  Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Sauti ya Umma SAU katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 pamoja na Mgombea Mwenza Bi. Satia Bebwa mara baada ya kuchukua Fomu hizo katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa  leo jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Mutamwega Mgaiwa kupitia Chama Cha Sauti ya Umma SAU katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akisaini Kitabu mara baada ya kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles 

Mgombea Mwenza kupitia Chama Cha Sauti ya Umma SAU Bi.Satia Bebwa akisaini kitabu katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk.Wilson Mahera Charles

Mgombea wa Urais ,Queen sendiga akikabidhiwa Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Allance for democratic change ADC katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Queen sendiga akionyesha  Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Allance for democratic change ADC katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 mara baada ya kuchukua Fomu hiyo  katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Queen sendiga kwa tiketi ya Allance for democratic change ADC katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akisaini Kitabu mara baada ya kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles 

Mgombea wa Urais , Twalib Kadege akikabidhiwa Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kupitia chama cha  United People’s Democratic Party (UPDP) katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Twalib Kadege wakionyesha  Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha  United People’s Democratic Party (UPDP) katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 pamoja na Mgombea Mwenza Ramadhani Ali Abdallah mara baada ya kuchukua Fomu hizo katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa  leo jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Twalib Kadege kupitia chama cha  United People’s Democratic Party (UPDP) katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akisaini Kitabu mara baada ya kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles 

…………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya  chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa, ametoa mpya mara baada ya kwenda  kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo akiwa miguu.

Hata hivyo amesema kuwa sababu kubwa iliyompelekea kuchua fomu akiwa hivyo ni ishara ya  utetezi wao kwa wakulima kwa kuwa hakuna anayelima akiwa na viatu.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya walipowasili  katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma, wakiwa peku hali iliyozua maswali na mshangao kwa watu waliokuwepo katika maeneo hayo, huku wao wakitaja vipaumbele vyao kuwa lengo lao ni kumuinua mkulima kwa kuhakikisha anauza mazao yake kwa bei yenye tija.

“Sisi ni watoto wa wakulima na mkulima halimi na viatu na ndiyo mwenye shida, kuna Watanzania wengi mpaka leo hawana viatu, sisi ndiyo watetezi wa wanyonge tunataka vipaumbele vyetu viwe ni amani, upendo na umoja cha pili ni kilimo tunataka tumkomboe mkulima apate bei nzuri ya Pamba kwa 5000, Korosho 5000 na Kahawa ni 5000 kwa kilo” amesema  Mgaywa.
Muttamwega Mgaywa pamoja na mgombea mwenza Satia Mussa wamejitokeza  kuchukua fomu ya kuwania Urais katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.