Home Michezo Uwanja wa Michezo Dodoma kubeba mashabiki zaidi ya Elfu 80

Uwanja wa Michezo Dodoma kubeba mashabiki zaidi ya Elfu 80

0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi  akiwa katika Studio za Dodoma FM Redio  Jijini Dodoma leo asubuhi, kuzungumzia Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa Miaka Mitano katika Kipindi Maalum, ambapo alikuwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Bw. Bilson Vedastus (hayupo pichani). Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi  (Kushoto) akiwa katika Studio za Dodoma FM Redio  Dodoma leo asubuhi, kuzungumzia Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa Miaka Mitano katika Kipindi Maalum, ambapo alikuwa na mtangazaji wa kipindi hicho Bw.Pius Jayunga (kulia).Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi  (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja watangazaji wa Dodoma FM Redio  mara baada ya kumalizika Kipindi Maalum cha kuzungumzia Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitano kilichofanyika leo katika Studio hiyo Jijini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mtangazaji Pius Jayunga, wapili kushoto ni Mtangazaji wa Kipindi  Zania Miraji na  wa kwanza kulia ni Lucas Godwin.

*************************************

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dodoma

06/08/2020.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi asema uwanja utakaojengwa eneo la Nzuguni Dodoma utakuwa mkubwa kuliko viwanja vyote nchini na utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki zaidi ya elfu themanini.

Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma alipokuwa katika Studio za Dodoma Fm Redio kuzungumzia Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano ambapo amesisitiza kuwa kama alivyoahidi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuwa atateleza ujenzi wa uwanja huo, taratibu zote zimekwishamilika na kuwasilishwa serikalini hivyo ni fedha tu ndiyo zinasubiriwa ili tenda ziweze kutangazwa, hii ni adhima ya serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

“Kwa suala la kuendeleza viwanja serikali imekuwa ikiwasihi wamiliki kuviendeleza viwanja hivyo na kwa Dodoma uwanja wa Jamhuri unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi na Serilaki imekwisha zungumza nao kuhusu kuboresha uwanja huo na tuliwaeleza pale watakapohitaji wataalamu wa masuala ya viwanja wizara inaweza kuwasaidia tunao wataalamu hao,”alisema Dkt. Abbasi.

Kwa upande wa Sekta ya Habari kuhusu Sheria ya Huduma  ya Habari ya 2016 Dkt. alifafanua kuwa lengo la sheria hiyo nikuifanya tasnia ya habari iheshimike zaidi na kuwa taaluma rasmi kama ilivyo taaluma ya wanasheria  na tunataka taaluma hii iendelee kukua zaidi.

Aidha, Dkt.Abbasi alibainisha kuwa sheria hiyo iliweka kiwango cha chini kwa Mwanahabari kuanzia ngazi ya Diploma na Serikali ilitoa kipindi cha miaka mitano cha Wanahabari kujiendeleza  na ukomo wake ni mwaka Disemba 31, 2021.

Halikadhalika Dkt.Abbasi alisema taifa limeingia katika uchumi wa kati ni heshima na jambo la kujivunia kwa watanzania wote hivyo hii itatoa fursa kwa serikali kuwa na uwezo mkubwa wa kukopa na kukopesheka kwa lengo la kuendeleza miradi mbalimbali na kama taifa lazma tuendelee kuchapa kazi, pia alitoa wito kwa watanzania kuwa watulivu katika kipindi cha uchaguzi.