Home Michezo  Mashindano ya Pool ya Kenice Nanenane kuanza rasmi leo.

 Mashindano ya Pool ya Kenice Nanenane kuanza rasmi leo.

0

Bingwa mtetezi wa mashindano ya Pool ya  Kenice nanenane, Baraka Jackson akicheza kwenye moja ya mashindano jijini Dar es Salaam.Refa wa kike wa mchezo wa Pool, Vaileti Mrema, akiwaamuru wachezaji Abdallah Husein(kulia) na Baraka Jackson katika moja na mechi walizowahi kucheza mwaka jana.

**********************************

MASHINDANO ya Pool kuelekea siku kuu ya Nanenane yanatarajiwa kuanza rasmi leo jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala kwa udhamini wa Kampuni ya kutengeneza meza za Pool ya Kenice.

Akizungumza na waandishi wa habari mwandaaji na mratibu wa mashindano hayo kwa kushilikiana na Chama cha Pool, Michael Machela alisema maandalizi yameshakamilika kwa asilimia miamoja hivyo kesho saa kumi jioni mashindano yanaanza rasmi.

Machela alisema, mashindano yam waka huu yatashirikisha timu za mikoa pamoja na mtu mmoja mmoja(singles).

Timu za mikoa shiriki mwaka huu ni pamoja na Mkoa wa kimichezo wa Temeke, Ilala,Ubungo Kigamboni, Kinondoni, Morogoro na Manyara.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja (singles), jumla ya wachezaji 128 wanatarajiwa kushiri mashindano hayo.

Aidha Machela alisema kutakuwa na ushiriki pia wa mchezaji mmoja mmoja(singles) wanawake ambapo jumla ya Wanawake 16 wamethibisha kushiriki.

Machela alizitaja zawadi za washindi pia kuwa bingwa wa wachezaji mmoja mmoja(Singles) Vijana atazawadiwa pesa taslimu shilingi 500,000/=, mshindi wa pili 100,000/= na mshindi wa tatu 50,000/=

Wachezaji mmoja mmoja(singles) Wakongwe bingwa atazawadiwa pesa taslimu shilingi 200,000/=, wa pili 100,000/= na watatu 50,000/=

Upande wa wanawake bingwa atazawadiwa pesa taslimu shilingi 50,000/= na wa pili 10,000/=

Upande wa timu Vijana bingwa atazawadiwa pesa taslimu shilingi 300,000/= na wa pili 100,000/=,  upande wa timu Wakongwe bingwa atazawadiwa 300,000/=

Bingwa mtetezi wa mashindano haya upande wa mchezaji mmoja mmoja(singles) ni Baraka Jackson kutoka Manyara.