Home Mchanganyiko Ajira 8771 zazaliwa Arusha

Ajira 8771 zazaliwa Arusha

0

****************************

Queen Lema Arusha

Imeelezwa kuwa jumla ya miradi 112 yenye thamani ya dola za kimarekani 570 imefanikiwa kuandikishwa kwenye mkoa wa Arusha ambapo pia katika kipindi cha miaka mitano hiyo jumla ya ajira 8771 ziliweza kuibuliwa kutokana na miradi na uwekezaji huo.

Pia katika mkoa wa Kilimanjaro jumla ya miradi 29 iliweza kuandikishwa ambapo miradi hiyo ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani 111.9 na iliweza kuibua ajira zaidi ya 1900 kwa kipindi cha miaka mitano.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (T I C) Kanda ya Kaskazini Bw.Daudi Riganda mapema jana kwenye viwanja vya maonesho ya  nanenane Themi  wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa watanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali hapa nchini

Alisema kuwa katika kipindi hicho cha miaka  mitano ndani ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kumekuwa na utofauti mkubwa sana wa kiuchumi kutokana na uwepo wa uwekezaji lakini pia miradiDaudi ambayo imekuwa ni fursa kubwa.

“Kwa mfano ndani ya mkoa wa kilimanjaro hiyo miradi 29 iliyoandikishwa miradi 9 ilikuwa ni ya wageni,miradi 8 ilikuwa ni ya ubia yaani wageni na wadhawa huku miradi mingine 12 ilikuwa ni ya watanzania hii ni hatua kubwa sana kwa watanzania na ninataka kusema kuwa bado fursa ni nyingi sana za uwekezaji hata ndani ya mkoa huu wa  kilimanjaro” aliongeza Daudi.

Katika hatua nyingine aliwataka watanzania kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kupiga hatua kila mara ikiwa ni pamoja na kufanya uwekezaji hali ambayo itaongeza zaidi mapato ya nchi ya Tanzania.

Alifafanua kuwa ni muhimu sasa kukusanya mapato na kama yakipanda basi ufanyike uwekezaji mkubwa kwa kuwa fursa ndani ya mikoa hiyo miwili ipo hata kwa kupitia katika kituo hicho cha uwekezaji.

“Ifike maali watanzania tuachane na tabia ya kulalamika kila mara,bali tusimamie na kuchangamkia fursa ambazo kila mara kituo hiki tunazitangaza kwa umma, tuachane na tabia ya kuwa wachuuzi kila mara” aliongeza.

Alihitimisha kwa kusema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia kituo hicho cha uwekezaji ipasavyo kwa kuwa wao wapo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini pia kuwasaidia wawekezaji wote kwa kufauta sheria na kanuni za nchi.