WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akifanya mazoezi ya kukimbia na watumishi wa TAMISEMI kabla ya kuwasilsha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akivishwa medali na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Maswala ya Afya TAMISEMI , Dkt. Dorothy Gwajima kama ishara ya kumpngeza kwa mafanikio ya miaka miaka mitano katika sekta ya Afya TAMISEMI leo katika viwanja vya Michezo Shule ya Sekondari Dodoma
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akitoa zawadi kwa mama aliyejifungua leo katika kituo cha afya cha Makole Jijini Dodoma
Baadhi ya watendaji kutoka mamlaka za Serikali za Mitaa katika sekta ya Afya wa kimfatila WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akiwa katika picha na mama aliyejifungua leo katika kituo cha afya cha Makole Jijini Dodoma
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati (kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole alipofika kuwaona wakina mama waliojifungua leo kabla ya kutoa mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma
Baadhi ya watendaji kutoka mamlaka za Serikali za Mitaa katika sekta ya Afya wa kimfatila WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumza wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akizungumza wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma.
………………………………………………
Na Alex Sonna, Dodoma
Serikali imesema uboreshaji wa Huduma ya Afya Msingi ni nguzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa kati kwani uimara wa afya za watanzania ndo chachu ya kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo na WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma.
Aidha katika hafla hiyo Waziri Jafo amejikuta akibubujikwa na machozi namna wananchi walivyo kuwa wakipata adha na kupoteza maisha kutoka na ukosefu wa huduma za afya kwenye baadhi ya maeneo nchini jambo lililokuwa linadhohofisha afya za wananchi katika utafutaji wao kutokana na kutokuwa na afya imara.
Waziri Jafo amesema kwa wananchi wengi wa likuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za afya, lakini kwa kipindi cha miaka mitano ya serikali chini ya Rais John Magufuli imetoa kipaumbele kwa sekta hiyo na kuondoa adha kwa wananchi hivyo kuchagiza katika utafutaji wa kipato .
“Kuna watu wenye uwezo hawa fahamu kwamba watanzania walikuwa wanateseka, walikosa kupata huduma bora za afya, na wanasafiri zaidi ya kilometa 140 kufua tahuduma za afya, kina mama wanapata matatizo ya fistula, baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu na vituo vipo mbali,” ameeleza Waziri Jafo.
Waziri Jafo ameongezea kuwa Watu hawafahamu kuna wakina mama wangapi wamekufa kwa kukosa huduma muhimu wengine wamesafirishwa kwa baiskeli na mikokoteni kufata huduma za afaya.
Waziri Jafo ameweka wazi kuwa watanzania wanaoishi mijini hawafahamu kama Taifa limepoteza watu wengi kwa kukosa huduma.
“Leo Rais Magufuli amekuja na maono mapana ya kuhakikisha anaokoa maisha ya watanzania kwa kuwasogezea hudumaza afya karibu na kutaka watendaji wa huduma za afya kutekeleza weledi wao kwa ufasaha kwa kutoa huduma bora kwa watanzania wote nchini bila upendeleo.
Aidha, Waziri Jafo amesema nchi tangu ilipopata uhuru hadi Rais Magufuli anaingia madarakani kulikuwa na Hospitali za wilaya 77 katiyaHalmashauri 185.
“Mpaka sasa kwa awamu ya kwanza hospitali 67 zimekamilika, zikaongezwa zingine na sasa jumla ya hospitali 99 zinajengwa, hizo za kwanza zimeanza kutoa huduma na hizo zingine zipo hatua mbalimbali ya ujenzi, tuna kila sababu ya kumshukuru Rais,”ameeleza Waziri Jafo.
Pia Waziri Jafo amesema zaidi ya zahanati 1198 zimejengwa kwa kipindi cha miaka mitano.
“Niwashukuru wataalam wangu, kwa kuwa wamekuwa ni injini ya kuhakikisha mambo yanasonga katika sekta ya afya, idara hii ilikuwa mfu lakini Rais ameibeba idara hii na sasa inafanyakazi katika ubora unaohitajika na watanzania,”ameshukuru Waziri Jafo.
Waziri Jafo amebainisha kuwa wakinamama wajawazito waliojifungua katika vituo hivyo vipya ni 219,764 na waliopata huduma ya upasuaji ni 18,826.
Huku Wagonjwa wengine wakiwemo kina baba zaidiya 6,000 wamefanyiwa upasuaji wa kawaida kwenye vituo hivyo, na kina baba wengine wametengeneza familia zao katika vituo hivyo, wazee zaidi ya 100,000 wamepata huduma,”ameweka bayana Waziri Jafo.
Lakini pia katika hatua nyingine Waziri Jafo ametembelea kitu cha afya cha Makole na Kutoa zawadi ya sabuni, maziwa na maji kwa wakina mama waliojifungua kwa siku ya leo akiwambia leo ni siku ya Afya TAMISEMI ikionyesha mafanikio yaliyofanyika ndani ya miaka mitano katika sekta ya afya hapa nchini.
Awali, Mwakilishiwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Grace Maghembe, amesema kuwa kuna mikoa mitano ili kuwa haina kabisa hospitali za rufaa za mikoa, lakini kwa sasa zimejengwa na zinatoa huduma katika ubora wa hali ya juu.
“Uboreshaji wa huduma za afya ikiwemo za kibingwa nchini umechangia kupunguza idadi ya wagonjwa wa kupelekwa nje ya nchi”, aesema Maghembe.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk.Dorothy Gwajima amesema kuwa uwepo wa miundombinu hiyo inatakiwa kwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ili kuwa vutia watanzania wengi zaidi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF).