Home Mchanganyiko WAUMINI WA DINI YA KISLAMU NCHINI KULIOMBEA TAIFA KUFANYA UCHAGUZI MKUU KWA...

WAUMINI WA DINI YA KISLAMU NCHINI KULIOMBEA TAIFA KUFANYA UCHAGUZI MKUU KWA AMANI NA UTULIVU

0

 

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodom, Mustapher Shaaban akitoa hotuba ya Swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma baada ya swala ya Eid.

Baadhi ya Viongozi wa Dini wakiongoza takibira kabla ya Swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma .

Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la BBC,Aboubakari Famau (kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mhariri wa Fullshangwe blog, Majid Abdulkarim na mbele ni Mtoto wake Famau baada ya Swala ya Eid iliyofanyika katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma.

Baadhi ya waumini wakifatilia kwa umakini hotuba ya swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi leo Jijini Dodoma.

Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la BBC, Aboubakari Famau (kwanza Kushoto) akisalimiana na Mhariri wa Fullshangwe blog, Majid Abdulkarim leo baada ya swala ya Eid katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma.

……………………………………………………..

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma

Waumini wa Dini ya Kislamu nchini wametakiwa kuliombea taifa kudumisha amani na utulivu uliyopo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika 28 Oktoba 2020 ili kuweza kupata viongozi bora , waadilifu na wazalendo katika kuwatumikia watanzania kwa kuleta maendeleo.

Wito huo umetolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodom, Mustapher Shaaban katika Msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma wakati wa swala ya Eid.

Sheikh Shaaban amesema kila mtanzania anawajibu wa kuliombe taifa ili kuhakikisha linalinda  amani na utulivu katika kuelekea Uchanguzi Mkuu ili viongozi watakao patikana kutokana na maombi ya watanzania wakasimamie katika kuleta  maendeleo ya taifa .

“Hivyo maombi hayo yatasaidia  kupata viongoz waadilifu,  wema , wanyenyekevu ,wanao sikiliza wananchi wao, wenye  uzalendo na kutatua kero za watanzania kwa wakati bila kuleta uvunjifu wa amani na mshikamano uliopo katika nchi yetu”, ameeleza Sheikh Shaaban.

Mbali na hilo Sheikh Shaaban amesema dini ya uislam inafundisha amani na mshikamano  hivyo ni vema kupeana ushirikiano kwa ustawi wa amani na maendeleo nchini ili kujenga taifa bora.

Aidha Sheikh Shaabani amewataka wamini hao kutumia siku ya Eid kuwaombea ndugu na marafiki wote waliyotangulia mbele za haki kusamehewa makosa yao yote kwa Mwenyezi Mungu na kusema mambo mazuri juu yao ili  kupata kauli thabit kwa Allah.

Pia Sheikh Shaabani amekumbushia kuwa leo ndo siku muhimu watu wanatakiwa kukaa na familia zao kwa kujumuika na kufanya ibada, ya kuchinja kwa wale wenye uwezo wa kuchinja na kutoa sadaka kwa watu wasio kuwa nauwezo ili kutimiza adhima ya siku kuu ya Eid.

Sheikh Shaabani amemaliza kwa kutoa pole kwa Taifa kwa kumpoteza Hayati Benjamini Mkapa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu na kusema kuwa waumini wa Dini ya Kislamu watamuenzi kwa mambo mengi ikiwemo Ujenzi wa Msikiti wa Gadafi ulijengwa kipindi cha Utawala wake na kipindi hicho  aliyatoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.

“Hivyo waumini tunamuenzi Hayati Mkapa kwa hayo mambo mawili makubwa kwani leo tumepata ibada yetu ya swala ya Eid hapa na watoto wetu wanaendelea kupata elimu Chuoni hapo na wanapomaliza masomo yao wanapata ajira na kulitumikia taifa”, ameweka wazi Sheikh Shaaban.