Home Siasa Rc Tanga Msimamizi Mkuu Mchakato wa kura za Maoni UVCCM-Manyara

Rc Tanga Msimamizi Mkuu Mchakato wa kura za Maoni UVCCM-Manyara

0

………………………………………………………………………

Na John Walter-Babati

Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa uwakilishi Bungeni katika  kundi la Vijana ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amewataka wajumbe kuchagua kiongozi atakaewatetea na kuepuka vitendo vya rushwa.

 Ametoa wito huo leo Julai 30,2020 mjini Babati linapoendelea zoezi la Mchakato wa kura za maoni kumchagua mwakilishi Ubunge  kundi la vijana  ambapo katika mkoa wa Manyara wagombea waliojitokeza ni kumi na tatu wajumbe 33 kati ya 34.

Wakijieleza wagombea hao mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la vijana na msimamizi mkuu wa mchakato huo, wameeleza namna watakavyowasaidia vijana katika kujinasua kwenye wimbi la ukosefu wa ajira kwa kuanzisha fursa mpya.

Aidha wameeleza kuwa matamanio yao makubwa ni Kutetea vijana kupata haki zao bila kubagua na Kuhakikisha nyumba za watumishi zinajengwa.