Home Michezo KLOSE AANZA MAZOEZI KWA MARA YA KWANZA KAMA KOCHA MSAIDIZI BAYERN MUNICH

KLOSE AANZA MAZOEZI KWA MARA YA KWANZA KAMA KOCHA MSAIDIZI BAYERN MUNICH

0

…………………………………………………………….

NA EMMANUEL MBATILO

Mfugaji wa Magoli muda wote michuano ya kombe la Dunia raia wa Kijerumani Miroslav Klose ameanza mazoezi kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Bayern Munich kama kocha msaidizi wa miamba hiyo ya mjini Munich.

Ikumbukwe Klose katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 kule Brazil alivunja rekodi iliyowekwa na Mshambuliaji wa Brazili Ronaldo De Lima aliekuwa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote katika michuano hiyo kwa kufikisha Magoli 15, hivyo Klose alivuka rekodi hiyo kwa kuweka kambani Magoli 16.