Home Mchanganyiko WANANCHI MAGU WAMLILIA MKUU WA WILAYA KERO YA KUSHAMBULIWA NA FISI

WANANCHI MAGU WAMLILIA MKUU WA WILAYA KERO YA KUSHAMBULIWA NA FISI

0
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Shishani baada ya kukgua miradi y maendeleo ya ujenzi wa jengo la RCH na  nyumba za waganga katika Zata ya Shishani jana.Picha na Baltazar Mashaka
…………………………………………………………………………………..

NA BALTAZAR MASHAKA,MAGU

MKUU wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, akikagua shughuli na miradi ya maendeleo amekumbana na kero ya wananchi wa Kijiji cha Nyasato, Kata ya Jinjimili wakilalamikia kushambuliwa na fisi hali inayotishia usalama na maisha yao.

Walitoa kilio hicho  kwa mkuu huyo wa wilaya kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana baada ya kukagua shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, elimu na maji.

Mmoja wa wananchi hao Maira Sanga akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema kuwa, maisha yao yako hatarini pamoja na familia zao kutokana na kushambuliwa fisi  na hivyo kujenga hofu kwa wananchi wa kijiji hicho.

“Mheshimiwa mkuu wa wilaya hapa tunakabiliwa na tatizo la wanyama wakali aina ya fisi  wanatishia uhai na maisha yetu pamoja na familia.Wanyama hao wamekuwa tishio kwenye jamii kutokana na kuwashambulia na kusababisha washindwe kufanya shughuli za uzalishaji,tunaomba serikali itusaidie kuwakabili na kuwapunguza,”alisema Sanga.

Alisema hivi karibuni kijana mmoja alishambuliwa na kung’atwa  fisi mguuni, familia moja nayo ilivamiwa usiku na fisi hao, pia wanyama hao waliwahi kuwashambulia watoto watatu wakiwa njiani kuelekea shuleni na kusababisha vifo vyao hivyo wamekuwa tishio kwa maisha ya wananchi na wakazi wa Kijiji cha Nyasato .

Akijibu kilio cha wananchi hao Kalli alisema atatoa kibali cha kuwapunguza ili wasiendelee kuleta madhara kwenye jamii na akatoa angalizo kuwa wasilalamike kuwa amepunguza nguvu kazi yao ya mashambani, hatawaelewa na wala serikali haitaki wananchi walalamike.

“Ndugu zangu na watani wangu Wasukuma tuwe wakweli, tukisha wapunguza mkilalamika baada ya zoezi hilo kuwa nimepunguza wafanyakazi wenu wa mashambani sitawaelewa,tutanaka watu wahangaike na mambo ya msingi si haya yanayohusu fisi,” alisema Kalli na kumwagiza Mkuuwa Polisi Wilaya ya Magu Mahamoud Banga kushirikiana na maofisa wa wanyamapori kutekeleza agizo.

Aidha Mrakibu huyo wa Mwandamizi wa Polisi aliwaambia wananchi hao kuwa zipo taratibu za kuwashughulikia wanyamapori wnaodhuru watu ingawa jeshi hilo haliamini ufugaji wa wanyama unaodaiwa kufanywa na kabila la Wasukuma .

“Kama mnawafuga wanyama hao (fisi) angalieni namna ya kuwahudumia lakini si kwa  kuwalisha binadamu na atakayebainika atachukuliwa hatua .Pia tuchunguze fisi hao wanaishi na wanapatikana wapi  na Afisa Mtendaji awasiliane na Ofisa Wanyamapori  waje kuwapunguza fisi hao,”alisema Banga.