Home Siasa WATAKIWA KUCHAGUA MGOMBEA MWENYE UWEZO

WATAKIWA KUCHAGUA MGOMBEA MWENYE UWEZO

0
Msimamizi wa mkutano wa Kura za maoni kutafuta mgombea wa udiwani kata ya Mtwivila,Theresia Mtewele akiongoza mkutano huo
 Baadhi ya watia Nia udiwani kwa tiketi ya Ccm kata ya Mtwivila Manispaa ya  Iringa
 Baadhi ya watia Nia udiwani kwa tiketi ya Ccm kata ya Mtwivila Manispaa ya  Iringa
Wajumbe wa kata ya Mtwivila wanisubiri kupiga kura ya kuchagua mgombea ambaye atawawakilisha nafasi ya udiwani.
…………………………………………….
NA DENIS MLOWE, IRINGA
WAJUMBE wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mtwivila wametakiwa kuchagua mgombea ambaye atawawakilisha vizuri vizuri kwenye Baraza la madiwani na kuwaletea maendeleo.
Akizungumzia wakati wa mkutano maalum wa upigaji Kura za maoni za kutafuta mwikilishi wa kugombea udiwani wa kata ya Mtwivila kwa tiketi ya CCM , mjumbe wa halmashauri Kuu Ccm taifa, Theresa Mtewele alisema kuwa wajumbe ndio wenye uwezo wa kumchagua mgombea mwenye uwezo katika kata na kukiwakilisha vyema chama kwenye uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa wajumbe ndio wenye Mamlaka ya kupata mgombea ambaye atasababisha CCM kuweza kupata kura nyingi kutoka kwa  mgombea ambaye ana nguvu kwa jamii na kufanya kuibuka na ushindi wa kishindo.
Alisema kuwa wagombea wote waliojitokeza wana Nguvu sawa lakini uchaguzi sahihi wa mgombea toka ngazi ya chini itasababisha ngazi ya ubunge na urais kuwa rahisi kuibuka na ushindi wa kishindo.
Mtewele alisema kuwa endapo chama kikikosea kwenye ngazi za chini Basi Hali huwa ngumu kwenye nafasi nyingine hivyo natoa wito kumchagua mgombea ambaye ana nguvu kubwa kwenye jamii
Alisema kuwa wajumbe wanatakiwa kuchagua mgombea bila kujali dini,ukabila kwani ndani ya CCM wanachama wote ni sawa hivyo mgombea atakayepitishwa kwenye kura za maoni aungwe mkono na wagombea wote.
Aliongeza kuwa CCM imejipanga vyema kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu hivyo chugueni mtu sahihi kwa ajili ya maendeleo ya kata ya Mtwivila.