Home Siasa PROF KITILA MKUMBO APONGEZWA NA WAHITIMU WA 2017 TOKA SHULE KUU YA...

PROF KITILA MKUMBO APONGEZWA NA WAHITIMU WA 2017 TOKA SHULE KUU YA ELIMU (SOED) CHUO KIKUU CHA DSM.

0

*********************************

Na Hamis Abeid Baruani

Baada ya siku chache kupita tangia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Ubungo kumuamini Prof Alexander Kitila Mkumbo kwa kumpa kura nyingi za kutosha kuongoza katika kinyang’anyilo hicho.

Kura hizo nyingi alizozipata Prof Kitila Mkumbo ni kura za maoni za kumpendekeza kuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Ubungo ambapo kura hizo za maoni zitasaidia vikao vya uteuzi kufanya uteuzi wake.

Wahitimu mbali mbali waliopita mikononi mwa Prof Kitila Mkumbo toka Shule Kuu ya Elimu (SOED) Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii na sehemu nyingine nyingi kumuunga mkono mwalimu wao na kufurahishwa na uaminifu wa wajumbe kwa mwalimu wao Prof Kitila Mkumbo.

Prof Kitila Mkumbo alikuwa ni mwalimu wa masomo ya saikolojia ndani ya shule kuu ya elimu Chuo Kikuu Cha DSM ambapo alihudumu hadi 2017 kabla ya kuaminiwa na Mhe Rais Ndg Dr John Joseph Pombe Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Wahitimu hao ambao ni wanafunzi wake wameahidi kumuunga mkono kwa kila hatua itakayofuatia ikitokea vikao vya uteuzi vitapendekeza jina lake kuwa mgombea wa CCM jimbo la Ubungo.