Home Mchanganyiko WAZEE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWATUNZA

WAZEE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWATUNZA

0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu, akikagua makazi ya wazee Msufini mkoani Tanga alipotembelea kwa lengo la kuona maendeleo ya makazi hayo.

Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee Msufini Anna Mgelwa kilichopo Wilayani Muheza mkoani Tanga akisoma taarifa ya Makazi hayo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya – Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipotembelea kwa lengo la kuona maendeleo ya makazi.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na Wazee katika makazi ya Mwanzage na Msufini Mkoani Tanga alipotembelea kwa lengo la kuona maendeleo ya Makazi hayo. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimiana na Mzee Elias Shija katika makazi ya Wazee ya Mwanzage Mkoani Tanga, alipotembelea makazi hayo

Mmoja wa wazee katika makazi ya Msufini, akitoa burudani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu kushukuru juhudi za Serikali katika kuwahudumia wazee wasiojiweza nchini.

………………………………………………………………………….

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJW

Na Mwandishi wetu Muheza

Wazee wanaoishi kwenye makazi ya Mwanzage na Msufini Mkoani Tanga wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kuwatunza na kuhakikisha wanapata mahitaji yao muhimu.

Hayo yamebainishwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika makazi hayo yenye lengo la kuona maendeleo ya uendeshaji wa vituo hivyo.

Mzee Flolian Michael amesema kuwa Serikali iliyo chini ya Rais Magufuli imekuwa ikiwajali sana wazee wasiojiweza nchini kwa kuwekea miumdombinu rafiki na kuwapatia huduma muhimu za malazi chakula na matibabu.

“Tunaishukuru Serikali ya Magufuli, tunapata chakula, tunavaa, Mungu ambariki” alisema.

Naye Mzee Milton John ameomba kuangaliwa zaidi kwa kundi la wazee wasio na walezi  kwani wamekuwa wakipatwa na matatizo mbalimbali na kukosa msaada kabisa.

“Nimshukuru Rais Magufuli kwa kutukumbuka wanyonge tusio na waangalizi hasa sisi wazee endelee kutukumbuka wanyonge” alisisitiza

Akizungumza mara baada ya kukagua Makazi hayo Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewahakikishia wazee hao kuwa Serikali itaendelea kuwatunza na kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuongeza watumishi kwenye makazi yao.

“Serikali inawapenda, ina jukumu la kuwatunza ikiwemo kuwapa matibabu, tunayo Sera ya matibabu bure kwa wazee ambayo mnaipata, tunaelewa kuna vipimo vya ziada na hilo ni jukumu letu kugharamia” alisema.