Home Michezo YANGA YASIMAMISHWA NA MWADUI FC

YANGA YASIMAMISHWA NA MWADUI FC

0

Na Mwandishi Wetu, 
Yanga SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Sare hiyo inawafanya Yanga SC wafikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 36 na kuendelea kukamata nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa tayari, Simba SC wenye pointi 81 za mechi 35.
Katika mchezo wa leo, Yanga SC walitangulia kwa bao la kiungo wake maradadi, Feisal Salum Abdallah ‘Fe Toto’ dakka ya 26 akimalizia pasi ya mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa.

Mwadui FC ambayo inafikisha pointi 41 baada ya mchezo wa 36 leo na kuabaki nafasi ya 15, ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Yahya Mbegu aliyefunga dakika ya 56 akimalizia pasi ya Omary Daga.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Juma Abdul/Paul Godfrey ‘Boxer’ dk46, Adeyum Ahmed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Kelvin Yondan/Abdullaziz Makame dk73, Mrisho Ngassa/Erick Kabamba dk60, Feisal Salum, David Molinga/Yikpe Gislain dk60, Ditram Nchimbi/Patrick Sibomana dk73 na Deus Kaseke.
Mwadui FC; Mussa Mbisa, Frank John, Yahya Mbegu, Khalfan Mbarouk, Augustine Samson, Mussa Chambega, Wallace Kiango, Gerlad Mathias/Markiad Mazela dk87, Raphael Aloba/Enock Jiah dk62, Venence Ludovic/Malik Jaffar dk87 na Omar Daga.