Home Burudani USIKU WA “IAM ZUCHU” HISTORIA YAWEKWA

USIKU WA “IAM ZUCHU” HISTORIA YAWEKWA

0

Muonekano wa Ukumbi kwa nje katika onesho la Zuchu lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam Muonekano wa Lady Jaydee kwenye show ya Zuchu Dayna Nyange akiwa kwenye red carpet katika show ya Zuchu Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Tessy na Dullvani kwenye red carpet show ya Zuchu. Modo wa kimataifa toka Tanzania Flaviana Matata akiwa na designer Ally Remtullah kwenye red carpet show ya Zuchu.

Khadija Kopa kwenye show ya Zuchu Single mama Shilole akiwa na Kaka yake wa kufikia Baba Levo wakifurahia katika show ya Zuchu Wema Sepetu kwenye show ya Zuchu Muonekano wa Queen Darleen kwenye show ya Zuchu Kwa mtazamo wako amenoga au amepuyanga.Muonekano wa Zuchu kwenye show yake wapongezwa kila konaKatibu Mkuu wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas akisalimiana na Msanii Rayvanny katika onesho la Zuchu lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas akisalimiana na Meneja wa Diamondplatnamz Salaam SK katika onesho la Zuchu lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas akiongea na Msanii Diamondplatnamz katika onesho la Zuchu lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Katibu Mkuu wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas akizungumza na mashabiki mbalimbali waliohudhuria katika onesho la “Iam Zuchu” lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Mwanamuziki Zuchu maarufu “I AM ZUCHU” akiimba katika onesho lake la kwanza tangu aanze kuimba muziki lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhutiwa na mamia ya mashabiki wake. Mwanamuziki Mbosso akitumbuiza katika onesho la Zuchu lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Msanii Zuchu (Kushoto) akiwa na Diamondplatnamz (Kulia) wakipiga picha ya pamoja kwenye Sanamu la Zuchu katika onesho la “Iam Zuchu” lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.Baadhi ya wapenzi wa Muziki na Mashabiki wa Zuchu , waliohudhuria Usiku ‘Special’ kwa ajili yake ,wakifurahia Performance zinazoendelea Juu ya Stage katika onesho la Zuchu lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Tamasha la ‘IAM ZUCHU” ni moja la Tamasha la burudani tunaweza kusema limeweza kuweka historia katika kiwanda cha burudani hapa nchini,limekuwa la aina yake kwa wale walioweza kupata fursa kuhudhulia na kushuhudia tamasha hilo.

Viongozi wa Serikali pia waliweza kufika katika tamasha hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam wakiwemo Katibu Mkuu wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas, Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Wasanii wakubwa pamoja na mastaa wakubwa hapa nchini pamoja pia waliweza kufika katika tamasha hilo wakiwemo, Juma Jux, Dullvanny, Wema Sepetu,Shilole,LadyJaydee,Dulla Makabila, Flaviana Matata na wengine wengi.

Akizungumza katika Tamasha hilo Zuchu amewashukuru wapenzi wa burudani hapa nchi pamoja na wale waliowezesha tamasha hilo kufanyika hivyo ameahidi kufanya makubwa kwenye tasnia ya muziki na kuweza kufika mbali kwenye tasnia hiyo.

“Nawashukuru Watanzania Kwa Upendo wenu Mkubwa , kwa mapokezi ya Kimalkia na kunifanya niwe msanii ninaetazamwa zaidi kwasasa Afrika Mashariki”. Amesema Zuchu.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akitoa neno kwa niaba ya Serikali amesema Serikali inathamini sana Sanaa ndio maana imemuagiza awe katika tamasha hilo, Lakini pia yeye binafsi ni Shabiki mkubwa wa @wcb_wasafi.