Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini miaka ya 1975 – 1980 Philemon Mgaya, wakati wa serikali ya awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Marehemu Philemon Mgaya alifariki dunia 14/07/2020 katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 20/07/2020 Usangi, Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kusho) akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omari Mahita, wakati walipoenda kutoa pole nyumbani kwa familia ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini miaka ya 1975 – 1980 Philemon Mgaya, Bahari Beach jijini Dar es salaam. Marehemu Philemon Mgaya alifariki dunia 14/07/2020 katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 20/07/2020 Usangi, Mwanga mkoani Kilimanjaro. Picha na Jeshi la Polisi.