Home Siasa WATIA NIA UDIWANI VITI MAALUM WAFIKIA 109 DODOMA MJINI

WATIA NIA UDIWANI VITI MAALUM WAFIKIA 109 DODOMA MJINI

0

………………………………………………………………………..

Idadi ya Wagombea wa Udiwani Viti Maalum jijini Dodoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) imefikia 109 huku zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu likitamatishwa siku ya leo.

Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa amesema zoezi hilo linaenda vizuri ambapo muamko wa wanawake kuchukua fomu ni mkubwa na unaonesha jinsi gani Demokrasia ndani ya CCM imepamba moto na watu wanavutiwa kufanya kazi ya kumsaidia Rais Magufuli.