Home Mchanganyiko BALOZI SOKOINE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNDP

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNDP

0

Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akisalimiana na
Bi. Christine Musisi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) mara baada ya mkutano baina yao uliofanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais
Mtumba – Dodoma. Pamoja na mambo mengine mkutano huo umejadili namna ya
kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira.

Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia) akiwa
katika kikao pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) ukiongozwa na Bi. Christine Musisi ambae ni Mwakilishi Mkazi. Kikao hicho
kimelenga kuimarisha ushirikiano katika hifadhi ya Mazingira hususan katika maeneo ya
Mabadiliko ya Tabianchi, Uchumi wa Bahari, Nishati endelevu, Hifadhi ya Bioanuai na
Ikolojia. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba – Dodoma.

Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa katika
picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
ukiongozwa na Bi. Christine Musisi – Mwakilishi Mkazi mara baada ya kukamilika kwa
kikao cha mashirikiano baina yao. Wengine katika picha ni wataalamu kutoka Ofisi ya
Makamu wa Rais na UNDP

Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akiagana na Bi.
Christine Musisi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) mara baada ya kukamilika kwa mkutano baina yao uliojadili namna ya
kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira. Mkutano huo umefanyika katika
Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba – Dodoma.