Home Siasa ZAIDI YA WANAWAKE 22 WAJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE VITI MAALUM RUVUMA

ZAIDI YA WANAWAKE 22 WAJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE VITI MAALUM RUVUMA

0

 Katibu wa umoja wa wanawake(UWT)Mkoa wa Ruvuma Rukia Mkinda kushoto akikamkabidhi  mjumbe wa kamati ya utendaji wa Chama cha  Walimu(CWT)Taifa Mwalimu Sabina Lipukila  kulia ya kugombea Ubunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma.

,Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Ruvuma Anifa Chingumbe kulia akipokea fomu ya kugombe Ubunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma kutoka kwa Katibu wa umoja wa wanawake mkoa wa Ruvuma Rukia Mkindu katika ofisi ya Uwt mkoani humo.

Mgombea Ubunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Happines Ngwando kulia akipokea fomu ya Ubunge kutoka kwa katibu wa umoja wa wanawake mkoa wa Ruvuma Uwt Rukia Mkindu ambapo hadi kufikia jana jumla ya wanachama 22 wa umoja huo wamejitokeza kuchukua fomu ya Ubunge wa viti maalum.

…………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu,Ruvuma

ZAIDI ya wanawake 22 wamechukua  fomu  ya kuwania nafasi ya ubunge wa  Viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Ruvuma ikiwa ni idadi kubwa zaidi kwa wanawake kujitokeza kugombea nafasi hiyo katika mkoa huo.

Katibu wa Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT)Mkoa wa Ruvuma Rukia Mkindu amesema kuwa wakinamama wanaendelea kujitokeza katika uchukuaji wa fomu hizo na kuwa hadi sasa ni zaidi ya 20 wamechukua na wengine wameshazirejesha.

 Mkindu amesema kuwa kabla ya kuwakabidhi fomu hizo wagombea hao wanapewa maelekezo mbalimbali ikiwemo na namna ya ulipiaji wa fomu hizo kuziingiza kwenye akaunti husika na kisha kukabidhiwa fomu na kuzijaza.

 Baadhi ya waliochukua fomu hizo kuwa ni Sabina Mbena Lipukila ambaye amechukua saa 4:26 asubuhi ni mwalimu anatokea Chama Cha Walimu (CWT) na wengine ni Happiness Ngwando ambaye tayari fomu yake ameshairejesha saa 4:38 asubuhi ,mhandisi Anifa Chigumbe ambaye ameschukua saa 4:10.

 Wengine ni Habiba Mfaume Asiya na Upendo Ndunguru  hao ni  sehemu ya baadhi ya waliochukua fomu kuwania nafasi hiyo huku katibu wa Jumuiya hiyo amewataka wachukuaji fomu hao kuzingatia maagizo yaliyowekwa na chama ili yasifanyike makosa katika ujazaji fomu hizo.

Hata hivyo idadi hiyo inaweza kuongezeka kwani muda wa kuchukua fomu bado upo na utamalizika tarehe 17 Mwezi huu na kuwataka wanachama wa jumuiya hiyo kujitokeza kuchukua fomu za kuomba kugombea Ubunge wa viti maalum.