Home Mchanganyiko VIONGOZI WA KIISLAMU LETENI MAENDELEO MNAPOPATA NAFASI

VIONGOZI WA KIISLAMU LETENI MAENDELEO MNAPOPATA NAFASI

0
Naibu Khalifa wa Wilaya ya Mwanga Hamad Dauti maarufu kwa jina la Kitobo akifafanua Jambo kwa Viongozi wa Twariqa ambao hawapo Pichani katika Uchaguzi huo.
Msemaji wa Twariqa Tanzania  Shekhe Haruna Hussein katikati aliyesimama akizungumza na Wajumbe wa Uchaguzi katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Twariqa Tanzania.
……………………………………………………………………………………
NA.Mwandishi Wetu – Mwanga.
Viongozi wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuacha malumbano yasiyo na tija na kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo kwa Waislamu Pindi ambapo wanapatiwa nyadhifa Mbali Mbali.
Akizungumza wakati wa Uchaguzi wa Khalifa Wilaya ya Mwanga Msemaji wa taasisi ya Twariqa Tanzania Shekhe Haruna Hussein alisema kuwa Wakati umefika wa viongozi wa dini kuacha mazoea na kuhakikisha kuwa wanaleta tija katika maeneo yao badala ya kubaki wanalumbana bila sababu.
Shekhe Haruna alisema kuwa waisalamu wanahitaji maendeleo na sio kubakia kwenye hitma na ziara tu,Bali maendeleo na mabadiliko makubwa badala ya mafarajano.
“ndugu zangu Waislamu kazi yeyote Ile unayopewa na Waislamu Ni lazima uifanye kwa weledi,na ujue kuwa unatumikia watu na sio kazi ya kulala nyumbani tu,Sasa Ni lazima tuwe na vitega uchumi vingi na vitusaidie na sio kudidimiza dini”alisema Haruna.
Aidha aliongeza kuwa ni lazima viongozi hao wajitambue na kufahamu kuwa wametoka wapi,wapo wapi na wanakwenda wapi ili kundi ambalo wanaliongoza liweze kujiendesha na kujitambua kwakuwa Twariqa inayohitajika Sasa ni ambayo itakuwa inapiga hatua za kimaendeleo.
Nae Khalifa wa mkoa wa Kilimanjaro Amin Khatibu amewataka viongozi kutambua kuwa uongozi ni changamoto na kazi hiyo ni ya Mungu,hivyo wachukue dhima kwa Mungu kuongoza watu wake.
“Kazi yeyote mnayopewa Ni lazima mtambue kuwa lazima mtumikie watu na muwe na hekma Sana katika kuunganisha watu na ambao hawatapata nafasi ya washirikiane na waliopewa dhamana ili kuhakikisha dini inasogea na maendeleo yanapatikana.”alisema Khatibu
Uchaguzi huo wa uongozi wa Wilaya ya Kitwariqa Mwanga katika ngazi ya Wilaya ambapo jumla ya wagombea watatu ambao katika nyadhifa ya khalifa wa Wilaya walichuana¬† Abdulkarim J.Mziray ,Mohamed Zaidi Ng’ido ambapo Shekhe Abdulkarim Mziray alipata Kura 08,na kutangazwa mshindi dhidi ya Mohamed Zaidi ambaye alipata Kura 04.
Nafasi ya Naibu Khalifa ilichukuliwa na Hamad Dauti (kitobo)ambaye alipita bila pingamizi.
Taasisi ya Twariqa Tanzania ilianzishwa mwaka 1932 ambapo ni taasisi Kongwe ya Kiislamu hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.