Home Mchanganyiko MKAZI WA DAR MIKONONI MWA MUROTO KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA BINADAMU KINYUME...

MKAZI WA DAR MIKONONI MWA MUROTO KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA BINADAMU KINYUME NA UTARATIBU

0

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP. Gilles Muroto akionyesha baadhi ya Dawa za Binadamu zilizokamatwa zikisafirishwa kinyume na utaratibu wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP. Gilles Muroto akionyesha namna dawa za binadamu zilizokamatwa zilivyokuwa zimefungwa na kusafirishwa kinyume na yutaratibu wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………….

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Fredrick Anaclet Maxmilian (38) mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma ya kusafirisha shehena ya madawa ya binadamu, sambuli 149 baadhi yakiwa na nembo ya MSD.

Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP. Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma.

Aidha Muroto amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 09/07/2020 majira ya saa moja jioni.

“Katika mahojiano ya awali mtuhumiwa amebainisha kuwa yeye sio daktarin wala siyo mfamasia wa dawa”, ameeleza Muroto.

Muroto amesema kuwa mtuhumiwa huyo anashirikiana na mfamasia ambaye ni mtumishi wa serikali huko mkoani Tabora.

Muroto amesema kuwa mtuhumiwa dawa hizo ameleta Dodoma kwa ajili ya kuuza katika maduka binafsi ya dawa.

Lakini pia Muroto ameongeza kuwa uchunguzi bado naendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

“Nitoe wito kwa watanzania kuwa waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kutokomeza uharifu wowote katika nchi yetu, lakini pia tutumie miiko na maadili ya taaluma zetu katika utendaji wa kuleta maendeleo na kujenga taifa hili”, ametoa wito Muroto.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Samweli Seseja ameeleza kuwa katika shehena hiyo dawa zilizo kamatwa na mtuhumiwa huyo ni dawa aina 8 zenye nembo ya serikali na zilikuwa ziingie sokoni na kusababisha hasara kwa serikali.

“Mtuhumiwa huyo amekamatwa na dawa na baadhi ya vifaa tiba ambapo alikuwa akivisafirisha kinyume na taratibu za usafirishaji wa dawa hizo kwani kila dawa zina kipimo cha joto lake hivyo nyingine zahitaji kuwa katika jokofu ili kulinda ubora wa dawa hizo”, amebainisha Dkt. Seseja.

Katika hatua nyingine Dkt. Seseja ametoa wito kwa wafanya biashara wa maduka ya madawa kununua dawa kutoka katika katika vyanzo sahihi na vilivyopewa mamlaka na serikali ili kulinda afya za watanzania na taaluma ya afya kwa ujumla.