Home Burudani DAIMOND,ALIKIBA NA HAMONIZE WAMPAGAWISHA RAIS MAGUFULI

DAIMOND,ALIKIBA NA HAMONIZE WAMPAGAWISHA RAIS MAGUFULI

0

 

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  kwenda kumtunza Mwanamuziki Ali Kiba hayupo pichani wakati wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM walipoalikwa Ikulu ya Chamwino jijin Dodoma kushudua ujenzi wa jengo la Ikulu mpya.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-IKULU CHAMWINO DODOMA)

Msanii Diamondplatnamz akiwatumbuiza wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM kushuhudia ujenzi wa jengo la Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Msanii Ali Kiba akiwatumbuiza wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM kushuhudia ujenzi wa jengo la Ikulu Chamwino jijini Dodoma.akiwatumbuiza wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM kushuhudia ujenzi wa jengo la Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Msanii Mwana FA akitumbuiza katika hafla hiyo.  

Msanii ADiamondplatnamz akiwa na wasanii wenzake kutoka WCB kwa ajili ya kunogesha tairi hii.

 

 

Meneja wa Diamondplatnamz Said Fella akiwa amekaa na msanii Zuchu ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho walipotembelea Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Julai 12, 2020

………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

WASANII wa mziki wa Bongo fleva wamempagawisha Rais John Magufuli katika hafla ya chakula cha mchana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) iliyofanyika Ikulu ya Chamwino.
Katika hafla hiyo, wasanii mbalimbali akiwemo Alikiba, Daimond Platnumz, Hamonize, Nandy, Zuchu, MwanaFA, Lavalava, kundi la Magufuli Gang likiongozwa na Shetta, Dogo Janja, Mrisho Mpoto, Bob Haiza,Rayvanny, Mbosso,Marioo, kundi la TOT na wasanii wengine, ambapo walipata fursa ya kutumbuiza na kukonga nyoyo za wajumbe wa mkutano huo.
Akizungumza namna alivyofurahishwa na mziki wao, Rais Magufuli amesema yeye ni shabiki sana wa nyimbo na huwa anafurahi sana.
“Nawashukuru sana wasanii kweli nimejisikia raha, unapomuona Alikiba amekaa pamoja na Daimond wamekaa pamoja unaiona nguvu ya CCM, leo unapomuona Harmonize aliyemkimbia Daimond anamsifia hadharani huu ndo utanzania ninao utaka, nawashukuru sana wasanii, asanteni sana kwa kuunga mkono Chama cha Mapinduzi,”amesema.
Amewataka waendelee kuitangaza Tanzania wasikate tamaa na kuwahakikishia siku zijazo mambo yatakuwa vizuri.
“Huwa nafurahi na nafuatilia kweli sijui nyimbo za Nandy za nani, endeleeni kuitangaza Tanzania, msikate tamaa tupo pamoja na nyinyi, endeleeni kukinadi Chama cha Mapinduzi, nataka kuwahakikishia siku zinazokuja mambo yatakuwa mazuri zaidi, nawashukuru mameneja wenu wote nawashukuru na waigizaji na wanamichezo wote kwa kazi kubwa ya kutangaza nchi yetu,”amesema.
Ameongeza “Kitendo mlichoonesha leo mkaoneshe hivyo hivyo, mapatano mliyofanya leo yakapate na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ninyi ni vijana mmeanza vizuri nendeni hivyo na Mungu atawajalia zaidi.”