Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Victoria Mlele akimfanyia uchunguzi wa afya Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Tanzania Meja Jenerali George William Ingram mara baada ya kutembelea banda la hospitali hiyo
************************
Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga nchini Meja Jenerali George William Ingram ametembelea banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga &Mloganzila) katika maonyesho ya 44 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba na kupongeza juhudi zinazofanywa na Muhimbili katika utoaji wa huduma za afya.
Meja Jenerali Ingram amesema hatua ya kutoa huduma bila malipo hii ni ya kupongezwa kwani inatoa fursa kwa wananchi kuonwa na wataalam na kupatiwa huduma .
Huduma zinazotolewa katika banda la Muhimbili ( Upanga na Mloganzila) ni uchunguzi wa macho , saratani ya matiti pamoja na huduma za dharura , ambapo kwa wale wanaobaonika kuwa na matatizo wanapatiwa rufaa kwenda Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kupatiwa matibabu stahiki.