Home Michezo KUMEKUCHA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE RATIBA YATOKA MAN UNITED KUKUTANA NA COPENHAGEN...

KUMEKUCHA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE RATIBA YATOKA MAN UNITED KUKUTANA NA COPENHAGEN AU BASAKSEHIR

0

Manchester United itamenyana na Copenhagen au Istanbul Basaksehir katika Robo Fainali ya  Europa League PICHA ZAIDI SOMA HAPA

……………………………………………………………………

TIMU ya Manchester United itamenyana na ama Copenhagen au Istanbul Basaksehir katika Robo Fainali ya UEFA Europa League ikiwa wataitoa LASK.
Man United pia inaweza kukutana na Wolves katika Robo Fainali itakayohusisha tmu za England tupu.
Wolves, wao wana mchezo mgumu wa Robo Fainali dhidi ya ama Sevilla au Roma ikiwa wataitoa Olympiacos kwenye hatua ya 16 Bora.

RATIBA KAMILI EUROPA LEAGUE

Robo-Fainali:
Wolfsburg / Shakhtar Donetsk vs Frankfurt / FC Basel 
Manchester United / LASK vs Istanbul Basaksehir / FC Copenhagen  
Inter Milan / Getafe vs Bayer Leverkusen / Rangers
Olympiacos / Wolves vs Sevilla / Roma
Semi-finals:
Mshindi RF 4 vs Mshindi RF 2
Mshindi RF 3 vs Mshindi RF 1 

Rangers watakutana na Inter Milan au Getafe kwenye Robo Fainali kama watapindua kipigo cha 3-1 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Bayer Leverkusen.
Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kimetanguliza mguu mmoja Robo Fainali baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya LASK ya Austria kwenye mchezo wa kwanza mwezi Machi.
Mechi yao ya Robo Fainali dhidi ya ama Istanbul Basaksehir ya Uturuki au Copenhagen ya Denmark itachezwa Agosti Ujerumani. Basaksehir inaongoza 1-0 baada ya mechi ya kwanza.

Wakati huo huo, Wolves walitoa sare ya 1-1 na Olympiacos ya Ugiriki mwezi Machi, lakini watakuwa na Robo Fainali ngumu dhidi ya Sevilla au Roma, ambao bado hawajacheza mechi hata moja kutokana na kusimama kwa mashindano hayo kwa sababu ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya coron