Home Mchanganyiko MHANDISI WARDA MESHAMERK AIPONGEZA SERIKALI KUTOA FURSA KWA WAHANDISI WA NDANI

MHANDISI WARDA MESHAMERK AIPONGEZA SERIKALI KUTOA FURSA KWA WAHANDISI WA NDANI

0

Mkurugenzi wa Kampuni ya Geared Consulting Engineers ltd warda Meshamerk akizungumzia namna serikali ya awamu ya tano ilivyotoa fursa kwa wahandisi wa ndani kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

************************************

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Ushauri wa masuala ya umeme ya (GEARED Consulting Engineers LTD) Mhandisi warda Ester Meshamerk ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fursa kwa wahandisi wa ndani nakuamini kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

Amesema katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano serikali imetambua uwezo mkubwa walionao wahandisi wa ndani nakutoa fursa ya kuwapa miradi mbalimbali mikubwa kuitekeleza hapa nchini.

Mkurugenzi Ambaye ni Mhandisi na mtaalamu mshauri wa masuala ya umeme warda aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa haabri .ambapo alisema anaipongeza Sana serikali kwa kuwaamini huku akitolea mfano kampuni yake kupewa mradi mkuwa wa Hospitali ya Kwanga iliyopo Msoma mkoani Mara.

“Wazawa tunapewa fursa tena kubwa katika kipindi hiki hakuna longolongo kwani ukikidhi vigenzo vyao tu unapata kazi bila shaka yeyote .mfano mimi licha ya miradi mingine mingi lakini serikali imeniamini na hivi Sasa kupitia kampuni yangu tunasimamia mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Kwanga unaoendelea katika eneo la umeme.”alisema Mhandisi warda

Nakuongeza kuwa “Najitahidi kuukimbiza mradi ule ili uweze kukamilika mapema ili wananchi wa mkoa wa Mara na viunga vyake waweze kupata huduma pale.amesema

Pia alisema licha ya kusimamia miradi mbalimbali hapa nchini lakini pia kampuni yake kutokana na kazi nzuri inazofanya imeweza kuaminika na kupata kazi katika nchi jirani Kama vile Malawi,Zambia na kungineko na hata Visiwani Zanzibar.

Wakati huohuo Mhandisi warda alisema kwakuwa kampuni yake moja ya kazi zake ni kusanifu Miundombinu ya umeme, na katika kuhakikisha vijana wanasoma masuala ya Ushauri hususani kwenye eneo la umeme wanaiva vizuri ameandaa semina ya kuwapiga msasa vijana hao ambao wako vyuoni.

Alisema semina hiyo itafanyika Julau 16 katika ukumbi uliopo DIT kwa maana Dar es Salaam Information Teknoloji ambapo vijana kutoka vyuo mbalimbali watakutanishwa hapo ili kuweza kupata madini mbalimbali katika sekta ya umeme .

“Semina hii italenga kuwapa ujuzi,na hasa wa kujua mabadiliko ya nyaya za umeme .miundombinu mingine kuhusu umeme hivyo semina hii itafanyika julai 16 pale DIT na lengo kubwa nikubadilishana uzoefu.na hasa kujua sokoni kunanini na chuoni kunanini.”amesema Mhandisi warda

mkurugenzi alimaliza kwa kuwataka vijana hao wakitanzania kuchangamkia fursa hiyo kwani watakuja kupata elimu ya kutosha hususani katika eneo la umeme.