Home Mchanganyiko ML 612 KUMALIZA KERO YA MAJI MILONJI

ML 612 KUMALIZA KERO YA MAJI MILONJI

0

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wa pili kulia akiangalia kisima cha maji kinachotumika kupeleka maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Milonji kata ya Lusewa wilayani Namtumbo mara baada ya kuzindua rasmi mradi mkubwa wa maji katika kijiji hicho,kulia meneja wa wakala wa maji vijijini RUWASA wilaya ya Namtumbo David Mkondya na wa pili kushoto Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Stephen Mashauri.Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akijaribu kuendesha baiskeli itakayomika na mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia maji kijiji cha Milonji kata ya Lusewa wilayani Namtumbo kwa ajili ya kusoma ankara za maji kwa wateja waliounganishiwa huduma ya maji safi katika maeneo yao ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu  ya tano kusogeza huduma hiyo karibu na makazi ya wananchi.

Picha na Mpiga Picha Wetu

*******************************

Na Mwandishi Wetu,
Namtumbo

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme,amezindua  rasmi mradi wa  maji katika Kijiji cha Milonji kata ya Lusewa wilaya ya Namtumbo uliojengwa na wakala wa maji vijijini  Ruwasa kwa gharama ya shilingi milioni 612,810,670.70

Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo, Mndeme amewataka wananchi wa Milonji kutunza miundombinu ya maji ili iweze kudumu kwa muda mrefu, na kuwaagiza viongozi wa serikali ya kijiji kushirikiana na kamati ya watumia maji kusimamia  kikamilifu mradi huo ili wananchi waweze kupata huduma muda wote.

Aidha Mndeme,ameipongeza Ruwasa wilaya ya Namtumbo kwa kukamilisha  ujenzi wa mradi huo ambao unakwenda kuleta nafuu  na kuboresha maisha kwa wananchi wa kijiji  hicho.

Alisema, kukamilika kwa mradi wa maji Milonji na miradi mingine inayotekelezwa katika wilaya ya Namtumbo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi yam waka 2015  inayolenga kumtua mama ndoo kichwani na kupunguza umbali wa kwenda kutafuta maji.

Mkuu wa mkoa alisema, lengo la serikali kutoa fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza mradi  huo ambao ulishindwa kukamilika kwa muda mrefu na kusogeza upatikanaji wa huduma ya maji karibu zaidi nawananchi wake na kupunguza muda ambao walikuwa anatumia kwenda kutafuta maji safi na salama mbali na makazi yao.

Amewaagiza viongozi wa serikali  ya kijiji, kutoruhusu watu kufanya shughuli zozote za kibindamu katika chanzo na eneo hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kuwachukulia hatua wale watakaonbainika kufanya shughuli tofauti na lengo la Serikali ikiwemo kilimo na kuchungia mifugo.

Kwa upande wake,memeja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo Davi Mkondya alisema, mradi wa mji kijiji cha Milonji chanzo chake ni kisima kirefu na maji yake yanakusanywa kwa nguvu ya jenereta inayotumia mafuta ya diesel.

Alisema, mradi huo ulitekelezwa na mkandarasi M/S Beras Investments Co Ltd mwaka 2013 na umekamilika mwaka 2015 kwa gharama ya shilingi milioni 612,810,670.67 na unahudumia zaidi ya wananchi 4,988 wa kijiji cha Milonji.

Mkondya alisema, katika utekelezaji wake kazi zilizopangwa kufanyika ni uchimbaji kisima,nyumba ya pampu na jenereta,kuchimba mitaro,ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 100,kujenga vituo 30 vya kuchotea maji.

Mkondya alimweza Mkuu wa mkoa kuwa licha ya  mradi huo kuna manufaa makubwa kwa jamii,  lakini unakabiliwa na changamoto ya mwamko mdogo wa baadhi ya wananchi katika kuchangia mfuko wa maji.

Hata hivyo alisema, katika kukabiliana na changamoto hiyo Ofisi ya Ruwasa wilaya  kwa kushirikiana na wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya wanaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuchangia mfuko wa maji.