Home Mchanganyiko SEKONDARI KOROGWE ZAJIPANGA VYEMA NA TAHADHARI YA CORONA

SEKONDARI KOROGWE ZAJIPANGA VYEMA NA TAHADHARI YA CORONA

0

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Mlangai akinawa maji tririka yaliyowekwa nje ya darasa kabla ya kuingia ndani.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mlangai wakiwa wamekaa kwa kuzingatia vigezo vya umbali wa mita moja kama walivyopangwa na walimu wao.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bungu wakiwa wanatoka darasani wakati wa Mapumziko.

Madarasa ya shule ya Sekondari Mlangai yakiwa yamewekewa vifaa vya kunawia maji tiririka.

…………………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu, Korogwe

Ikiwa ni wiki Chache Tangu kufunguliwa kwa shule za Msingi na Sekondari nchi nzima mara baada ya kufungwa kutokana na tishio la homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Covid 19 Shule za Sekondari Korogwe zimejipanga kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
Mwandishi wetu amepata kutembelea baadhi ya shule za sekondari zilizopo pembezoni mwa Wilaya hiyo za Bungu na Mlangai na kukuta utaratibu wa kunawa mikono na vipeperushi umezingatiwa huku Changamoto ikiwa ni kwenye uvaaji wa barakoa kwa wanafunzi.
Degratius Mapima ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mlangai hapa anaeleza namna walivyoweza kuandaa vifaa na mazingira ya kujisafisha kabla ya kuingia darasani.
“Tuliwapa elimu siku ya kwanza tu walivyoingia shuleni jinsi ya kujikinga, ikiwa kunawa mikono kila wakati na matumizi sahii ya barakoa” anasema mapima.
Anasema kama shule wameweza kuweka  vifaa vya kunawia kila mlango wa darasa na eneo la geti la kuingilia shuleni.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Bungu, Mohamed Mkono ametaja kuwa licha ya kuweka tahadhari zote lakini bado kunachangamoto ya wanafunzi kutovaaa barakoa .
“Licha ya tahadhari tulizoziweka bado tunachangamoto ya Wanafunzi wengi hapa awavai barakoa licha ya kuwaambia pia tatizo la social distance bado ni tatizo kwa vijana wetu kama unavyojua watoto wetu wanapenda michezo ya kukaribiana ndio maana hata kwenye kazi za makundi unawakuta wapo karibukaribu hivyo aiepukiki” anasema Mwalimu Mkono.
Anamaliza kwa kusema kuwa kicha ya changamoto ya kukaa nyumbani kwa takribani miezi mitatu wanafunzi walirudi shule wakiwa na hamasa kubwa mno tofauti na mika ya nyuma ambapo shule zikifunguliwa ukuta wanafunzi wanachwlewa.