Home Mchanganyiko WATIA NIA JIMBO LA NKENGE WAFIKIA WATANO, WAONYWA KUKUTANA NA WAJUMBE

WATIA NIA JIMBO LA NKENGE WAFIKIA WATANO, WAONYWA KUKUTANA NA WAJUMBE

0

…………………………………………………………………………………

Na Allawi Kaboyo, Missenyi

Baada ya chama cha mapinduzi kuwaruhusu watia nia wote kwa nafasi za ubunge na udiwani kuanzia tarehe 01,julai mwaka huu kuanza kupitapita, Katibu wa chama hicho wilaya ya Missenyi Ndg. Emanuel Alex amewaonya watia nia na wagombea kutofanya mikutano na wajumbe ambao ndio wapiga kura.

Alex ametoa onyo hilo julai 05,2020 kwenye ofisi za chama hicho alipofatwa na waandishi wa habari kwa lengo la kutaka kujua mchakato unaendaje kwa sasa baada ya wagombea kuruhusiwa kupita, alieleza kuwa watia nia waliruhusiwa kupita kwenye ofisi za chama wilaya na kata kwaajili ya kupata utaratibu na si vinginevyo.

“Chama kiliruhusu watia nia kupita kwenye ofisi za chama wilaya kwa watia nia ya ubunge na ofisi za chama kata kwa watia nia ya udiwani, lengo chama kilitaka watia nia hao kujitambulisha kwa viongozi na kupewa utaratibu wa chama katika uchukuaji wa form, gharama za form na masuala mengine. Ila niwatahadhalishe kuwa kauli hiyo haikuwaruhusu watia nia kukutana na wajumbe wa mkutano mkuu ambao ni wapiga kura nah ii hairuhusiwi na atakayebainika chama kitamchukulia hatua.” Alisema katibu huyo.

Ameongeza kuwa hadi tarehe hiyo watia nia ambao wamefika ofisini kwake wamefikia watano ambapo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kuwania uongozi mbalimbali kwakuwa vijana ndilo taifa la leo na kesho na kuongeza kuwa gharama za kuchukulia form kwa upande wa ubunge ni shilingi laki moja huku form ya udiwani ni shilingi elfu kumi.

Alex amesisitiza wananchi wa wilaya hiyo kutojihusisha na vitendo vy uvunjifu wa Amani katika kipindi chote cha uchaguzi kikiwemo kipindi cha kampeni na kuwasihi vijana kutokubali kutumika na wanasiasa kwa lengo la kufanya vurugu.

Mmoja ya watia nia aliyekutwa katika ofisi hizo Ndg.Evance Kamenge aliwaeleza waandishi wa habari kuwa ameamua kutia nia ya kugombea ubunge kwa lengo la kuwasemea wananchi wa wilaya Missenyi na maeneo yake kwa kuwa wamekosa msemaji sahihi kwa kipindi kirefu.

Kamenge alisema kuwa katika kipindi kirefu rushwa imekuwa ikiwanyima haki wananchi wa Nkenge kwasababu ya wabunge kuwa wale wale na kushindwa kuwatumikia wananchi wao kwa kuangalia kero zinazowagusa wananchi yakiwemo maji,umeme,barabara,kilimo na biashara mambo ambayo amesema tayari ameyafanyia upembuzi na kulipata suluhisho lake.

“Nimefika hapa baada ya kuangalia watia nia wote ndipo nilipoona nafaa kugombea na kuwatumikia wananchi wa Nkenge na Missenyi kwaujumla, wananchi wa Missenyi wanataka Maji, wanataka elimu juu ya kulima kilimo biashara na kufuga kisasa, wananchi wanataka mazingira ya kuwawezesha kufika mahali kwa kuwapa elimu lakini pia kuwasemea, wilaya yetu ipo mpakani hivyo tunazo fursa nyingi za kufanya biashara ya mpakani na kuimarisha uchumi wetu.” Alisema Kamenge.

Aidha Kamenge aliongeza kuwa katika kampeni zake hatarajii kuzungumzia mtu wala masuala ya mtu binafsi na badala yake ataongelea ataongelea mambo yanayowahusu watu na mahitajio yao ambapo pia amewasihi watia nia wenzake kutokuchafuana kwa lengo la kutafuta vyeo na kuchaguliwa.

“Katika kamepeni zangu zote sitomuongelea mtu wala masuala binafsi au kumchafua mtu, nitajikita kuzungumzia wananchi wanataka nini na kwa wakati gani, hivyo niwaombe wagombea wenzangu tusichafuane tukumbuke sisi sote ni watoto wa baba mmoja ambaye ni CCM na tunataka kuwatumikia watanzania hivyo tujikite katika kuzungumzia masuala yanayowagusa wananchi moja kwa moja.” Alisistiza Kamenge.

Wilaya ya Missenyi inajumla ya kata 20 ambapo kwasasa chama kinafanya mchakato wa kusambaza form za kugombea udiwani kwa kata zote huku wagombea udiwani wakiruhusiwa kupita na kupata taratibu.