Home Mchanganyiko WAKUU WA MIKOA WAPEWA MIEZI MIWILI KUFUATILIA FEDHA ZILIZO KWEPESHWA KATIKA MIFUMO...

WAKUU WA MIKOA WAPEWA MIEZI MIWILI KUFUATILIA FEDHA ZILIZO KWEPESHWA KATIKA MIFUMO YA SERIKALI

0

…………………………………………………………………………..

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Waziri Nchi, Ofis ya Rais, Tawla za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ametoa miezi miwili kwa Wakuu wa Mikoa yote nchini kufuatilia fedha zilizopotea ikiwemo fedha za makusanyo ya mapato ambazo fedha hizo hazikufikishwa katika mifumo ya serikali.
Agizo hilo ameltoa leo wakati wa kuwakaribisha wakuu wa mikoa wapya, wakuu wa wialaya wapya na wakurugezni waliyo teuliwa hivi karibuni.
Aidha Mhe.Jafo amesema kuwa kuna fedha za miradi na fedha za makusanyo katika mikoa hiyo hazikufikishwa katika mifumo ya serikali hivyo wahusika wachukuliwe hatua na fedha hiyo kurudishwa katika mifumo ya serikali ndani ya muda huo.
Mhe. Jafo amewataka viongozi hao kusimamia shilingi Bilioni 170 iliotolewa kwa ajiri ya kuimarisha na kukarabati miundo mbinu ya elimu nchini.
“Hivyo kahakikisheni mnasimamia kwa weledi mkubwa fedha hizo ili ndani ya miezi mitatu miundombinu hiyo iwe imekamilika na kuanza kutumiwa na wanafunzi wetu “amesisitiza Mhe. Jafo
Lakini pia Mhe. Jafo amewataka viongozi hao kutokaa maofisini tuu na badala yake watoke maofisini na kwenda kuwasikiliza wananchi na kujua wanashida gani na kuzitatua kwa wakati ili kutoleta kikwazo kwao katika shughuli zao za uzalishaji.
Mhe. Jafo amesisitiza kuwa kila mtu kuheshimu mipaka ya kazi yake ili kuleta ushirikiano mzuri katika kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi na kuimalisha mausiano mazuri na watendaji wote katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Naamini kila mmmoja katika nafasi yake akitimiza majukumu yake kwa kufata sharia na miongozo iliyoopo basi ni dhairi shairi tutaweza kujenga taifa hii na kuhacha alama kubwa katika vizazi vyetu vijayo”, AMESEMA Mhe. Jafo.
Naye Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga amesisitiza kuwa viongozi hao wanatakiwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao na kuimarisha utawala bora kwa kushirikiana katika kila hatua ya utendaji katika shughuli zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Polisi Thobias Andengenya amesema kuwa wamepokea maelekezo sasa ni kwenda kutekeleza kwa vitendo kwa kuhakikisha wanaziba mianya yote ya ubadhilifu ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa ufasaha kwa kuwaletea watanzania maendeleo.