Home Mchanganyiko DKT. NDUMBARO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA SABASABA

DKT. NDUMBARO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA SABASABA

0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika banda la Wizara Dkt. Ndumbaro amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi ili kuiletea sifa Serikali na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kimataifa.
“Kwa kuwa sisi tunafanya kazi ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nje na kuhakikisha mahusiano ya kimataifa yanaimarika hatuna budi kufanya kazi kwa bidii na maarifa yetu yote, hili ni jukumu letu hivyo ni lazima tuhakikishe tunalitekeleza kwa ufanisi na ufasaha,” Amesema Dkt. Ndumbaro.
 
Akiwa katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Dkt. Ndumbaro ametembelea pia banda la Bunge, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
 

 

Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, alipotembelea banda la Wizara katika maonesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.