Home Mchanganyiko KADA WA CCM ADESTINO MWILINGE AJITOSA KUGOMBEA JIMBO LA ISIMANI

KADA WA CCM ADESTINO MWILINGE AJITOSA KUGOMBEA JIMBO LA ISIMANI

0

 Kada wa chama chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa vijijini Adestino Mwilinge ajitosa kugombea jimbo la Isimani

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MBUNGE wa jimbo la Isimani
William lukuvu amenza kuupata upinzani ndani chama cha mapinduzi (CCM) mara
baada ya kada  wa chama hicho Adestino Mwilinge
kutangaza kutia nia ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea  ubunge wa jimbo hilo.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika kijiji cha Mbuyuni kada huyo alisema kuwa ameamua kutia nia kwa
mijubu wa kanuni na katiba ya chama hicho inavyosema kila mwananchama anahaki
ya kuchaguliwa na kuchagua kwa mujibu wa
ibara ya 14 (3) na 15 (1).
Alisema kuwa ameamua kutia nia
akiwa kijijini kwao kwa lengo la wadau watambue kuwa yeye ni mkazi wa jimbo la
Isimani na anania ya dhati ya  kusaidia
kuleta maendeleo kwa wananchi wanaishi katika jimbo hilo.
Mwilinge alisema ameamua kutia
nia baada ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr Bashir Ally Kakurwa
kutangaza wanachama wa chama hicho wanaruhusiwa kutia nia kwa kuwa ni wajibu
wao kulingana na katiba ya chama hicho.
Aliongeza kuwa anaunga mkono
juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuleta maendeleo ya nchi hii katika
kipindi hiki cha miaka mitano aliyokuwa madarakani.
Kada huyo aliyehudumu katika
chama cha mapinduzi kwa zaidi ya miaka kumi na tano akiwa katika uongozi wa
nyadhafa mbalimbali katika chama chake.
Mwilinge alisema kwa sasa
hawezi kueleza sababu iliyomfanya kuomba ridhaa ya kuomba kuteuliwa kuwa
mgombea wa jimbo la Ismani huku akiahidi kuweka wazi vipaumbele vyake muda
utakapofika.
Aidha Mwilinge alisema kuwa
wananchama wa chama cha mapinduzi wanawajibu wa kujilinda chama hicho kwa
kusimamia vizuri serikali na kusema mambo mazuri yanayofanywa na chama hicho.